Baadhi ya Wakazi wa mkoani njombe hawaifahamu sheria ya mtandao

BAADHI ya wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii Mkoani
Njombe wamesema kuwa sheria ya mitandaoni inayoanza kutumika Septemba Mosi
mwaka serikali ilitakiwa kuielimisha jamii hiyo juu ya madhara ya sheria hiyo.
Wakizungumza na kituo hiki walisema kuwa elimu juu ya sheria
hiyo haija wafikia na kuwa mpaka inaanza kutumika hawaelewi ni mambo gani
yanatakiwa kufanya na mabo gani hayatakiwi kufanywa katika mitandao ya kijamii.
Mmoja wa wakazi wa Mkoani Njombe Math Sanga alisema kuwa
anaishangaa sheria hiyo alivyo ielewa kuwa mtu akipokea picha anashitakiwa na
aliyeituma.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Mkoani humo wameiomba elimu
ingetolewa kwaza kabla ya kuaza kutumika na kuwa wanawasiwasi wa sheria hiyo
kuja kwaajili maalumu ya kuwabana watu wa upande fulani na kuwaachia watu
fulani.
Baraka Tave na Anjelo Mgaya wanasema kuwa
wanashauri sheria hiyo elimu ipite kwanza kwa jamii wanayo ipelekea sheria
hiyo.

from Blogger http://ift.tt/1N7PPns
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment