Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania Romana Tedeschi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha maeneo matano ya wazi ya Mji wa Zanzibar kwa kuanzia na Kiwanja cha Demokrasia Kibandamaiti utakaofadhiliwa na Shirika la SDC la nchi hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akizindua Mradi wa kuboresha maeneo ya wazi ya Mjini Zanzibar katika hafla iliyofanyika Idara ya Ardhi na Upimaji Forodhani Mjini Zanzibar, (kulia) Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Muhamad Juma.
Msaidizi Fundi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya Landscape ya Switzerland Roland Raderschall akitoa maelezo ya Mradi wa mwanzo wa kuboresha Kiwanja cha Demokrasia cha Kibandamaiti katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Zanzibar Muhamad Juma akitoa ufafanuzi kwa wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha eneo la wazi la Kibandamaiti., (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Mgharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
from Blogger http://ift.tt/1J4QE8X
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment