|
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Dkt. Jama Gulaid aliyemaliza muda wake wa Uwakilishi nchini.
Moja ya zawadi alizopokea kutoka kwa Balozi Mushy ni Kitabu kinachoelezea Vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyopatikana hapa nchini.
Pia katika mazungumzo yao, Balozi Mushy alimpongeza Dkt. Gulaid kwa kuiwakilisha vyema UNICEF hapa nchini. kwa Upande wa Dkt. Gulaid naye alitumia fursa ya kumshukuru Balozi Mushy kwa niaba ya Wizara na Serikali kwa ujumla kwa Ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chote cha uwakilishi wa UNICEF hapa nchini.
|
|
Balozi Mushy akizungumza na Dkt. Gulaid |
|
Dkt. Gulaid naye akizungumza huku Balozi Mushy akimsikiliza.(Picha na Reginald Philip). |
from Blogger http://ift.tt/1HpgPO1
via IFTTT
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment