PSPF TATOA VITANDA HOSPITALI YA TEMEKE VITANDA

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, imeisaidia hospitali ya wilaya ya Temeke, vitanda, magodoro na mashuka ili kusaidia serikali katika juhudi zake za kupunguza uhaba wa vifaa vya hospitali za umma.

Msaada huo ambao ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, alioutoa kwa uongozi wa PSPF, baada ya kutembelea hospitali hiyo wakati akiwa naibu waziri wa Sheria na Katiba, na kukuta akina mama wajawazito waliofika hospitalini hapo kujifungua wengine wakilala chini kutokana na uhaba wa viotanda, alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Abdul Njaidi na kuongeza PSPF, kwa kuwa ni Mfuko unaotoa huduma kwa jamii nao hauna budi kutoa sehemu ya faida na kuirejesha kwa jamii kwani wengi wao wanaofika hapo hospitali kwa ajili ya matibabu ni wanachama wa Mfuko na wengine ni wanachama watarajiwa wa Mfuko.

Kufuatia maombi hayo Mfuko huo umekabidhi vifaa hivyo leo Desemba 7, 2015, ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, alikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.

Akipokea vifaa hivyo katika hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Temeke, Photidus Kagimba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, aliishukuru PSPF, kwa moyo huo wa kusaidia jamii.

“PSPF mmeonyesha moyo wa uungwana kwa kusaidia akina mama zetu wakati wakisubiri kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala pazuri pa kulala.” Alisema.




Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (wakwanza kulia), akiungana na Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, (wapili kulia), mkurugenzi w manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Photidus Kagimbo, watatu kulia), mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, (wane kulia) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, (wakwanza kushoto), wakati PSPF, ikikabidhi msaada wa vitanda, mashuka na magodoro kwa hospitali hiyo, Desemba 7, 2015. Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mfuko baada ya kuombwa na Mh. Angela Kairuki.Na K-vis Media/Khalfan Said
Mbunge wa viti Maalum, Angella Kairuki, (wapili kulia), akipokea msaada wa vitanda, kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, kwenye hosptali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Desemba 7, 2015. Mfuko huo umetoa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka ili kuunga mkono juhudi za serikali za kumaliza tatizo la vifaa tiba kwenye hosipatli za umma. Kulia ni .. Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo. 
Njaidi (kulia), akiangalia wakati fundi akiunganisha moja ya vitanda hivyo wakati wa makabidhiano hayo.

from Blogger http://ift.tt/1NGqRXi
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment