SERIKALI ya mtaa wa Sido halmashauri ya mji wa Njombe na wachimbaji wadodo wa madini katika Jiwe kubwa ambalo wanaponda kokoto wametakiwa kufikia muafaka kabla hawaja nyang’anywa leseni ya uchimbani na kupewa mtu mwingine na ofisi ya madini mkoa.
Kauli hiyo imetolewa na mtaalamu wa madini Mkoa wa Njombe, John Maganga alisema kuwa serikali hiyo na waponga kokoto hao wafike muafaka wa kukata leseni kabla ofisi yake haijawapa watu wengine leseni ya uchimbaji wa madini katika eneo hilo na kuwa wachimbaji hao lazima wamshilikishe mmiliki wa eneo hilo ambaye ni mwenyekiti wa mtaa.
Katika eneo hilo kuna mgogoro ambao serikali ya mtaa inataka kuimiliki leseni ya uchimbaji wa madini ambayo wachimbaji hao wadogo wadogo wamelipia katika ofisi ya madini na kuendelea kuchimba kiharali bila serikali hiyo kujua.
“Nenda mahala popote ukitaka kukata leseni ya kuchimba madini ni lazima ukubaliane na mmiliki wa eneo husika ili kukata leseni ya eneo husika kama ni eneo la mtu binafsi awe amekuuzia eneo na ndipo ukate leseni,” alisema John
Alilisema kuwa wachimbaji hao wanacho takiwa kukifanya ni kufikia mwafaka na kuhusian ana leseni hiyo ili waendelee kuchima madini katika eneo hilo kwa kuwa wakiendelea na mgogoro huo ofisi ya madini ifafunga uchimbaji wa madini katika eneo hilo.
Siku za hapo nyuma waponda kokoto katika mtaa wa Sido eneo la Ganga Lyandefu kikundi cha Juakali kilifikiwa na wataalamu wa madini na kuwataka kuwa wakateleseni ambapo wananchi wa kikundi hicho walikata leseni yao bila kupitia kwa ofisi ya mtaa wao kitu kinacholeta mtafaruku.
Mtaalamu wa madini aliwaambia wananchi hao kuwa kwa kufanya hiyo kunamakosa yalitendeka kulipa pesa moja kwamoja bila kupitia kwa ofisi ya mtaa wao na hivyo kuomba lazi kwa kufanyika kwa kosa hilo.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo Richard Bimbiga alisema kikundi cha Juakali na wataalamu wa madini walikosea kufanya taratibu za kukata leseni bila kushirikisha serikali ya mtaa huo na kuwa eneo ambalo lipo jiwe hilo ni mali ya wakazi wote wa mtaa huo.
“Wachimbaji na wataalamu mlikosea sana kuto shirikisha serikali ya mtaa wenu wakati wa kukata leseni kwa kuwa jiwe hili na eneo mlilokatia leseni lipo katika mtaa na ni mali ya wananchi wote sasa mlivyo fanya sio vizuri hivyo mlitakiwa kushilikisha selikali ya mtaa,” alisemsa Bimbiga.
Wakitoa dukuduku lao katika mkutano huo ulio wakutanisha wachimbaji, Ofisi ya madini na serikali ya mtaa wachimbaji hao walisema kuwa katika mtaa kuna magali, kuna maduka lakini leseni za maduka zinapo enda kukatwa serikali haishirikishi.
Hivyo walisema kuwa hawapo tayari kuiruhusu serikali hiyo kwenda kukata leseni ya uchimbaji wa madini katika eneo hilo kwa kuwa serikali ya mtaa sio ninayo chimba katika eneo hilo.
Walisema hawairuhusu kwa kuwa kuna tetesi wanazipata kuwa serikali ya mtaa wao kuna muwekezaji wanataka kumkabidhi eneo hilo na wao kuwa chini ya muwekezaji huyo wanapo chima madini na mapato yao kuanza kumpa muwekazaji tofauti na ilivyo sasa wanacho kipata ni chao.
Mwenyekiti wa wachimbaji hao Raymond Mbuligwe ameunga mkono hoja za wachimbaji anao waongoza kwa kukataa leseni ya eneo lao kukaa ofisi ya mtaa huo na kuwa mmiliki ni wao na sio serikali ya mtaa.
from Blogger http://ift.tt/1m6GDVd
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment