CHADEMA KUELEKEA iKULU WAPIGWA MKWALA


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuelekea Ikulu jijini Dar es salaam kushinikiza kurejeshwa ka matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema Chama hicho kinatakiwa kutumia mbinu nyigine ya kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo hayo ya Televisheni ya Taifa na sio kupitia maandano.
Katika hatua nyingine jeshi hilo limesitisha kazi za vikundi vya ulinzi shirikishi katika kituo cha kati kutokana na kufanyika kwa vitendo vyenye harufu ya rushwa, kutofuata sheria za ukamataji pamoja na kutumia nguvu kupita kiasi huku Naibu Kamishna Siro akianisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kukamata wanaokiuka taratibu.

from Blogger http://ift.tt/1VWo9CG
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment