Zoezi hilo la upimbaji wa bure limeanza katika Hospitali ya Tanwatt halmashauri ya mji wa Njombe na katika eneo la kiwanda cha chai Kibena mkoani Njombe kwa lengo la kubaini viashiria vya maambukuzi ya ugonjwa wa kansa ya kizai inayo waasili wanawake na kupelekea vifo.
Akizungumzia zoezi hilo Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini ya Umati, Joseph Mwamwaja alisema kuwa zoezi hilo lipo mkoani Njombe na litaendeshwa kwa muda wa siku tatu katika hospitali ya Tanwatt na siku tatu katika eneo la kiwanda cha chai.
Dr. Mathias Mkyagila akitoa elimu kwa wakina mama |
Alisema kuwa zoezi hilo la uchunguzi linaendeshwa bure wa wakinamama ambao wanapatiwa elimu na kufanyiwa uchunguzi, na kupatiwa matubabu bure kwa watakao bainika kukutwa na viashiria vya ugonjwa huo.
Alisema kuwa zoezi hilo lilianza juzi Februari mosi na kukamilika Februari 3 katika hospitali ya Tanwatt ambapo wamelenga kuwafanyia uchunguzi wa wanawake 50 kwa siku na kuwa siku ya kwanza walifanikiwa kuwafanyia uchunguzi watu 42 na kubaini mwanamke mmoja mwenye viashiria.
Aliongeza kuwa kanda ya nyanda za juu kusini tatizo la ugungwa huo ni kama Tanzania nzima lilivyo kwa ukubwa wake hivyo jamii inahitaji huduma za kufanyiwa uchunguzi.
Aidha Daktari na mtoa nelimu kwa wanao patiwa huduma ya upimaji wa viashiria hivyo Dr.Matiath Mkyagila alisema kuwa zoezi hilo litawanufaisha wanawake kubaini mapema matatizo ya kansa ya shingo ya uzazi.
Alisema kuwa kwa mwanamke aliye fanyiwa uchunguzi kwa mara ya kwanza atapata uchunguzi tena kwa baada ya miaka mitatu na kwa ambaye atakuta na maambukizi ya Virusi vinavyo sababisha Ukimwi atarazimika kupima kila baada ya mwaka mmoja.
Alisema kuwa ugonjwa huo unasababishwa na mwanamke kuzaa watoto zaidi ya watano, kuwa na ushirikiani wa ngono na wanaime wengi.
Mmoja wa wanufaika wa upimaji huo na mfanyakazi wa Hospitali ya Tanwatt Ester Mgela alisem akuwa zoezi hilo limemuweka huru kwa kuwa amejua kuwa ni mzima na kuwa wanawake wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa madhara ya ugongwa huo ni makubwa na kuomba Umati kuhakikisha kuwa inapita mpaka vijijini ambako watu hao bado hawajapata elimu na hawakutwi na huduma za bure.
from Blogger http://ift.tt/1PYzs8K
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment