MAAMUZI MAPYA KESI YA ALIYE KUWA KAMISHNA MKUU WA TRA NA WENZAKE LEO APRIL 27 2016

April 01 2016 aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania, Shose Sinare walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja na kosa  la Utakatishaji fedha.

Kesi hiyo imeendelea leo April 27 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imefutilia mbali shitaka la utakatishaji fedha lililokuwa linawakabili washitakiwa wote  hivyo washitakiwa wamebaki na mashitaka saba.

Upande wa Jamhuri wamekata rufaa Mahakama Kuu na kusababisha maamuzi ya kupewa dhamana kuahirishwa mpaka April 29 2016 ambapo mahakama itatoa maamuzi kama watuhumiwa watapewa dhamana, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment