Wananchi walalamikia pesa za zahanati kuliwa na Mtendaji wa kijiji

WANANCHI wa kijiji cha Iboya halmashauri ya mji wa Njombe wameiomba ofisi ya mkurugenzi kushughulikia malalamiko yao yakiwemo ya ubadhirifu wa fedha zilizotokana na kuuza msitu kwaajili ya kukarabati jengo la zahanati ambalo hata sasa halijakamilika.
Wananchi hao wamesikitishwa na mwendo mzima wa utawala viongozi kijijini hapo ikiwemo utawala kibabe kwenye maamuzi ya pamoja kama uuzaji wa misitu na uvunjwaji wa kamati ya ujenzi wa zahanati.
Katika Kijiji hicho kuna changamoto ya kutosomwa taarifa za mapato na matumizi kwa takribani miaka minne pamoja na baadhi ya wananchi kunyanganywa misitu kwa kile kinachodaiwa kuwa misitu hiyo ni mali ya serikali ya kijiji pasipo maamuzi ya mkutano mkuu.
Hata hivyo zaidi ya shilingi milioni 8 fedha zilizotokana na kuuza miti ya mbao kwa lengo la kukamilisha ukarabati wa jengo la zahanati zinadaiwa kutafunwa na mtendaji wa kijiji hicho kwa kushirikiana na mwenyekiti wake pamoja na kamati ya kijiji.
Mmoja wa wananchi hao Forcus Mng’ong’o alisema pamoja na hayo wamedhamiria kumkataa mtendaji huyo kuendelea kuhudumu kijijini hapo kutokana na vitendo anavyo wafanyia Jambo ambalo linapingwa na uongozi wa halmashauri ya mji.
Alisema kuwa mpaka sasa Zahanati hiyo haiendelei na ujenzi kutokana na fedha zake kutafunwana Mwendaji wa kijiji hicho.

Alisema kuwa mtendaji alihamishwa kutokana na ubazilifu mahala pengine kabla ya kuhamia kijijini hapo.
Mtendaji wa kijiji cha Iboya Esio Mpete akizungumza kwa njia ya simu amekiri kuzitumia fedha za wananchi.
“Fedha za wananchi zilizo kuwa zimetengwa kwaajili ya zahanati baada ya kuuza msitu wa miti ya mbao zilipelekwa katika matumizi mengine,” alisema Mpete.
Tabia ya halmashauri kuwahamisha watendaji inapingana na maagizo ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ambae anawataka watawala kuwasimaisha kazi watendaji waovu.
Katika halmashauri hii kunautofauti ambapo kumeshuhudiwa na wananchi watendaji wakihamishwa baada ya kufanya ubadhilifu eneo moja na kuhamishiwa eneo jingine.
Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri ya Njombe mjini Edward Mwanzinga anawakingia vifua watendaji hao na kusema kuwa tarifa za ubadhilifu hazija wafikia ofisini.
Mwanzinga amewataka wananchi kutoa tarifa katika ofisi za halmashauri pale wanapo ona kuna ubadhilifu na kuwa katika uongozi wa halmashauri ya kijiji kuna viongozi wengi ambao wanaweza kuona ubadhilifu na kutoa taarifa.
“Unajua katika vijiji wananchi wanapenda kuchagua watu wasio na elimu ili kutoa walazimisha kufanya maendeleo ndio maana hata unapotokea ubadhilifu wanashindwa kutoa taarifa,” alisema Mwanzinga.

from Blogger http://ift.tt/23VKAN8
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment