Moja kati ya habari kubwa zilizoandikwa katika mitandao jana May 5 2016 ni kuhusiana na mipango ya Zimbabwe kutengeneza dola yao ili kukidhi uhaba wa fedha uliopo nchini.
Gavana wa benki kuu ya Zimbabwe John Mangudya ameeleza kuwa fedha ambazo zitakuwa kama dhamana ni dola milioni 200 ambazo wamepata support kutoka Africa Export-Import Bank.
Katika mpango huo Zimbabwe watatengeneza noti za dola mbili, tano, 10 na 20 ambazo zitakuwa na thamani sawa na dola ya Marekani. Kutokana na kushuka kwa thamani ya fedha yao Zimbabwe walitoa hadi noti ya dola bilioni tano “Unauliza mpango huo utakamilika lini?
tupo kwenye mchakato wa kushughulikia suala hilo ili kulikamilisha kwa sababu sio mpango wa usiku mmoja, bali unahitaji muda kwani fedha hizo zitaenda kuprintiwa nje ya nchi baada ya kazi ya kudesign kukamilika, fedha hiyo huenda ikatoka ndani ya miezi miwili ijayo”
Zimbabwe walianza kutumia rasmi dola ya Marekani mwaka 2009 kufuatia mfumuko mkubwa wa bei ambao ulikuwa endelevu. Tangu wakati huo wananchi wa Zimbabwe wamekuwa wakitumia dola nyingine za kigeni kama Rand ya Afrika Kusini na Yuan ya China.
0 maoni:
Post a Comment