Mei 6 2016 bunge linaendelea tena Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge wa Bukombe Doto Biteko ameuliza Serikali kuwa ‘Je, kwanini Serikali inachukua muda mrefu sana kurekebisha mishahara ya Walimu baada ya kupandishwa vyeo?‘
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya utumishi wa Umma na Utawala bora >>>’Ni kweli kwamba miaka ya nyuma kulikuwepo ucheleweshwaji wa kurekebisha mishahara kwa mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara wakati huo kila mwajiri kuwasilisha marekebisho ya watumishi wake Ofisi ya Rais‘
‘Kuanzia mwaka 2012 mfumo huu wa taarifa za kiutumishi na mishahara uliimarishwa kutoka toleo la 7 kwenda la 9 la Lawson ambapo mwajiri alisogezewa huduma ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kiutumishi yanayotokea katika ofisi yake bila ya kulazimika kusafiri kwenda Dar es salaam‘
‘Pamoja na utaratibu huu mzuri, mazingira machache yanayoweza kuchelewesha marekebisho ya mishahara kufanyika kwa wakati kutokana na kuingizwa taarifa za watumishi kwenye mfumo baada ya orodha ya malipo ya mishahara katika mwezi husika kufungwa‘ ‘Napenda kupitia Bunge hili, kuwataka waajiri wote kufanya marekebisho ili kuepusha ucheleweshaji wa haki za Watumishi.
0 maoni:
Post a Comment