Wapiga kura watapiga kura Ntarehe 8 Novemba kumchagua rais atakayemrithi Barack Obama wa chama cha Democratic.
Hapa
tutakupatia tathmini ya udadisi wa kura za maoni nchini humo, hasa
kuhusu ushindani kati ya mgombea wa Democratic Hillary Clinton na
mwenzake wa Republican Donald Trump.Baada ya mdahalo, huchukua siku kadha kabla ya matokeo yake kudhihirika kwenye kura za maoni.
Kura za maoni zina umuhimu?
Ni vigumu kubaini maoni ya watu zaidi ya 300 milioni lakini watafiti wa maoni bado hujaribu. Watu wanaotumiwa huwa ni 1,000 hivi na kwa kuzingatia maadili ya utafiti na sayansi, huwezekana kubashiri matokeo.Majimbo yanayoshindaniwa sana?
Kuna majimbo 13 ambayo yanatarajiwa kushindaniwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Hapa chini ni ramani ya majimbo hayo na uwezekano wa nani atashinda kwa kutumia matokeo ya kura ya maoni ya tovuti ya Real Clear Politics.
Ndipo Donald Trump aweze kupata nafasi nzuri, anahitaji kujishindia Florida na Ohio na majimbo mengine kadha. Kwa sasa hali ilivyo, Clinton yupo mbele kidogo Florida na Ohio.
Matokeo kamili ya kura za maoni za karibu majimbo hayo yanayoshindaniwa ni kama ilivyo hapa chini.
Trump na Clinton ndio wagombea pekee?
La hasha, kuna wagombea wengine wengi. Lakini wale wakuu ni Hillary Clinton na Donald Trump.
Mgombea wa Green Party Jill Stein, 66, ni daktari na mwanaharakati ambaye anatarajia kupata uungwaji mkono kutoka kwa wafuasi wa Democratic waliomuunga mkono Bernie Sanders ambao bado wanampinga Bi Clinton.
Gavana wa zamani wa New Mexico Gary Johnson, 63, anawania kupitia chama cha Libertarian Party na sana anaangazia kuwavutia wafuasi wa Republican wasiopendezwa na Bw Trump.
Kwa mujibu wa Real Clear Politics, Bi Stein ana karibu 2% ya kura naye Bw Johnson ana zaidi ya 7%.
Wawili hawa wanaweza kuchangia sana kuamua mshindi kwani watavutia wapiga kura kutoka kwa wagombea wakuu.
Clinton amefanya vyema?
Bi Hillary Clinton amepigiwa upatu kushinda lakini kuna wakati mwingine ambapo uongozi wake hupunguzwa sana. Majuzi zaidi ilikuwa mapema Septemba. Mwanzo, alionekana kuwakosoa wafuasi wa Donald Trump na kusema ni "kapu la watu wa kusikitisha" na wasioweza kuokolewa.
Baadaye, alionekana kukaribia kuzirai wakati wa sherehe ya ukumbusho wa shambulio la 9/11.
Umaarufu wake ulishuka kidogo lakini baadaye akajikwamua.
Trump aliongoza lini mwisho?
Wakati mmoja Trump aliachwa nyuma sana na Bi Clinton, akiwa nyuma kwa karibu 20% majira ya joto 2015 wagombea walipokuwa wengi. Hata hivyo, amefanikiwa kumpita Bi Clinton mara chache sana.
Mwisho ni alipopokea idhini ya kuwania urais mwisho wa Julai kwenye Kongamano la Taifa la Republican.
Hakuongoza kwa muda mrefu kwani mpinzani wake naye alijikwamua kongamano la Democratic lilipofanyika siku chache baadaye.
Wagombea wenza walisaidia?
Zamani wagombea wenza walisaidia sana, mfano Bill Clinton alipanda 12% baada ya kumteua Al Gore mgombea mwenza 1992.
Lakini karibuni mambo yamekuwa tofauti na mwaka 2016 hakujakuwa na mabadiliko makubwa.
Mgombea mwenza wa Trump, Gavana wa Indiana Mike Pence aliteuliwa Julai 15 naye wa Clinton, gavana wa zamani wa Virginia Tim Kaine akatangazwa Julai 22 July, lakini hakukutokea mabadiliko makubwa kwenye kura za maoni.
0 maoni:
Post a Comment