Uingereza ilianza msimu mpya chini ya kaimu mkufunzi Gareth Southgate kwa kupata ushindi dhidi ya Malta.
Swala
muhimu baada ya mechi hiyo kukamilika haikuwa ushindi uliopatikana bali
hatma ya Wayne Rooney na thamani yake katika kuichezea timu ya taifa ya
Uingereza,na iwapo mchezo ulioonekana ulipendwa na Southgate.Thamani ya Rooney katika timu hiyo ilikaguliwa kwa mara nyengine tena huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akiungwa mkono na mkufunzi huyo.
SouthGate alimwelewa Rooney na hakuelewa kwa nini mashabiki walipiga kelele baada ya mchezaji huyo kupiga juu wakati alipokuwa amesalia na kipa mwisho wa mechi hiyo.
Alisema: Inavutia kujua ni nini kinachoendelea katika maisha yake katika kipindi cha siku 10 zilizopita.Kila mjadala unamuhusu yeye.
''Mara nyengine anakosolea kwa maonevu lakini bado anaendelea kucheza na kujivunia taifa lake''.
Southgate alimfananisha Rooney na John Terry na Frank Lampard pamoja na Ashley Cole
0 maoni:
Post a Comment