HABARI MBALIMBALI KUTOKA NCHINI TANZANIA AMBAZO ULUSHWA NA GMCL FM 99.3 KATIKA KIPINDI CHA MBONI YETU SAA 3;00 USIKU KILA SIKU ZA JUMATATU MPAKA IJUMAA.



DODOMA

SERIKALI imemtaka waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu Jenista Mhagama pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordani Rugimbana kuiangalia  mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA kwa macho manne huku akiitaka mamlka huyo kuachakufanya kazi kwa mazoa.

Mwandishi wetu kutoka Dodoma Nazaeli Kirimbo ametutumia taarifa ambayo inasomwa studio na DOMINA ASANGALWISYE

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni harakati za serikali kuhamia Dodoma sambamba na kuifanya Dodoma kuwa jiji ambapo katika kufanikisha hilo mamlaka ya CDA inatajwa kuhusika kwa asilimia kubwa tokana na kazi yao upangaji wa miji. 

Insert……Mama Samia na DCA 

Ili kufanikisha zoezi hilo Makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mkoani dodoma mara baada ya ziara yake mjini Dodoma  akaitaka mamlaka hiyo kufanya zoezi la utanuzi wa mji wa dodoma. 
Insert…..Mama samua utanuzi wa mji 
Licha ya Manispaa ya Dodoma kudaiwa kuwa na maeneo madogo  makamu wa rais mama samia Suluhu Hassan akaitaka cda kushirikisha halmashauri za jirani ili kufanikisha zoezi hilo. 

Isnert….Mama samia kushirikisha majirani 

Jafari Mwanyemba yeye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma akatoa neno la shukrani kwa makamu wa Rais.

Insert……Jafari Mwanyemba

Wakati harakati hizo za kuifanya manispaa ya Dodoma kuwa kuwa jiji wananchi wanatakiwa kuwa tayari kupokea maoni ya mabadiliko kutoka kwa wataalamu kutokana na kuwa Dodoma imejengwa lakini haijajengwa kwa mfumo wa jiji, hivyo yapo mengi ambayo yatajitokeza ikiwa ni pamoja na maeneo mengine kubolewa na kufikia hadhi ya jiji.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxx

SONGWE
Wananchi wa mkoa mpya wa Songwe wameombwa kuanzisha miradi ya kiuchumi kwenye mkoa huo hususani kipindi hiki ambacho kunamahitaji makubwa ya huduma za kijamii na miundo mbinu.


DOMINA ASANGALWISYE

Mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya kukosa nyumba za watumishi,majengo ya huduma kama vile mahoteli na usafiri wa kuaminika tofauti na mkoa wa Mbeya.
Mbunge wa jimbo la Vwawa Jafeti Hasunga ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wananchi katika jimbo hilo waishio Dar es salaam ambapo katika mkutano huo suala la makao makuu ya mkoa huo linaonekana kuvuta hisia ya wananchi wengi.

INSERT…MBUNGE JAFETI

Kwa upande wao wananchi hao wamesema kuwa kuna baadhi ya wananchi wanasema wakiweka makao makuu vwawa watakosa biashara na wamesema wakifanya vitu visivyofaa basi watakosa maendeleo.
INSERT…WANANCHI SONGWE
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

SIMIYU
Hospitali teule ya mkoa wa Simiyu imepiga marufuku matumizi ya dawa za kienyeji za kuongeza nguvu ya uchungu kwa wajawazito ambazo zinaathali za kupasuka kizazi na kutokwa damu nyingi hali ambayo inaweza kusababisha kifo hivyo jamii inapaswa kukemia kitendo hicho.

ANTHONY FUZU

Hayo yamesemwa na mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa wa Simiyu Dk Fedrick Mlekwa alipotembelewa na ujumbe wa umoja wa madiwani wa CCM Tanzania waliofika hospitalini hapo kwaajili kutoa misaada katika wodi ya wakina mama na watoto.
Mlekwa amesema kuwa wajawazito wengi huuzulia katika zahanati na vituo vya afya na wanaojifungulia hositali ni wachache idadi kubwa hujifungulia majumbani jambo ambalo linaweza kusababisha vifo huku hospitali ikipiga marufuku wajawazito kuja na dawa za kienyeji za kuongeza uchungu.
INSERT…MLEKWA
Nao baadhi ya wagonjwa wameshukuru umoja huo kwa kutoa msaada walioutoa.
INSERT…WAGONJWA

Katibu wa UWAMA diwani kutoka manispaa ya Temeke Abdala Mtimika amesema moja ya kazi za umoja huo kufanya shughuli za kijamii hivyo wameamua kutembelea hospitali ya Somanda na kutoa misaada ya kibinadamu na zoezi hilo ni endelevu kwa nchi nzima.
INSERT…ABDALA

Misaada iliyotolewa na madiwani hao ni Khanga,sabuni za kufulia,mafuta ,kandambili,dawa za meno,juice na kandambili za kuogea na thamani yake ni kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
NJOMBE
Balozi wa Kenya hapa nchini Chelawa Ally Makwere ametoa wito kwa wafanyabviashara wa mikoa ya nyanda za juu kusini kwenda kuwekeza nchini Kenya kwa kuwa nchi hiyo kwa sasa inauhitaji wa uwekezaji katika sekta ya kilimo cha matunda,mashine za kusaga nafaka ikiiwa ni pamoja na mahindi na mpunga.

ANTHONY FUZU


Balozi Chelawa ametoa wito huo wakati wa mkutano wa wafanyabiashara wa Njombe ambao wanafanya biashara za nafaka ,matunda, mbao na kilimo cha chai.

INSERT…BALOZI WA KENYA

Pamoja na balozi huyo kuwaeleza wafanyabiashara maeneo mbalimbali yanayohitaji uwekezaji wafanyabiashara pia wamemueleza balozi changamoto zinazowakabili za kufanya biashara na wakenya kuwa ni kuzitelekeza bidhaa.

INSERT…WAFANYABIASHARA

Kabla ya kukutana na wafanyabiashara hao balozi alikutana na uongozi wa mkoa wa njombe ambapo akazungumza kuwa anataka kuimarisha mahusiano ya biashara.
INSERT…BALOZI WA KENYA 2

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
LINDI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed kuhakikisha hospitali ya wilaya hiyo inakusanya mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Antony fuzu

Ametoa agizo Oktoba 16, 2016  wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Lindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma.

INSERT…WAZIRI MKUU


Amesema taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo katika ukusanyaji wa mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000 hadi milioni nne kwa siku.

Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima.

Akizungumzia kuhusu matibabu kwa wazee, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Mohammed kuhakikisha anafungua dirisha la kuwahudumia wazee ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma wanapofika hospitalini hapo.


Naye Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Samwel Laizer amesema muamko mdogo wa jamii kujiunga na CHF ni moja kati ya changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma za afya.

Dk. Laizer amasema kati ya kaya 30,000 zilizoko wilayani Nachingwea ni kaya 7,133 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa CHF.

Awali Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Chuo Cha Walimu na kuwataka wabadilike ili waweze kuwatumikia wananchi kwa uadilifu bila ya kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.


XXXXXXXXXXXXXXXXXX

UKEREWE
Wilaya ya Ukerewe ambayo uchumi wake unategemea mazao ya uvuvi inampango mkakati wa kuongeza mapato yatokanayo na uvuvi kupitia uwekezaji wa ufugaji wa samaki ziwani.

DOMINA ASANGALWISYE

Hayo yamebainika kufuatia mazungumzo baina ya mkuu wa wilaya ya Ukerewe Estomi Chang”a na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ukerewe Frank Bahati baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanyika katika visiwa vya wavuvi wilayani Ukerewe.
Katika kile kinachoelezwa ni harakati za uboreshaji wa mapato kufuatia halmashauri kupewa jukumu la kuhakikisha zinakusanya zaidi ya asilimia 80 ya mapato vinginevyo zitafuutwa.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Ukerewe Frank Bahati amefunga safari kutembelea visiwa vya wavuvi kukagua shughuli zinazofanyika na kuzungumza na jumuiya ya wavuvi.

INSERT…FRANK


Akiwa amefuatana na afisa uvuvi na afisa masoko mkurugenzi mtendaji Frank Bahati amekagua baadhi ya shughuli zinazofanyika katika kisiwa cha Ghana ambacho ni maarufu kwa shughuli za uvuvi wilayani humo.

INSERT...CHANGAMOTO

Baada ya kukagua na kuzungumza na jumuiya za wavuvi Bahati akawa na mazungumzo na mkuu wa wilaya Esomi Chang”a na kuzungumzia namna ya kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa mazao ya uvuvi katika ziwa Victoria.

INSERT…MAZUNGUMZO

Asilimia 90 ya eneo la wilaya ya Ukerewe inazungukwa na maji ya ziwa Victoria hali inayofanya wilaya hiyo kutegemea shughuli za uvuvi kama chanzo kikuu cha mapato.
Hata hivyo katika siku za hivi karibuni biashara ya mazao ya uvuvi imekumbwa na kupungua kutokana na uvuvi haramu.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MWANZA

SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuhakikisha wanasajili mtumishi yeyote hata kama hana vyeti na ndani ya siku 14 mhusika huyo anatakiwa arejeshe vyeti vyake kwa Ofisa Utumishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema hayo katika ziara yake ya siku moja mkoani Mwanza ambapo alitembelea wilaya za Nyamagana, Misungwi na Ilemela.
Kairuki pia ameipongeza Nida kwa juhudi za kuendelea kusajili watumishi wa umma katika kuhakikisha wanapata vitambulisho vya taifa.
Amesema kila mtumishi wa umma anatakiwa kuhakikisha kuwa anapata Kitambulisho cha Taifa kabla ya Desemba mwaka huu na kuwashukuru wale wote waliojitokeza mpaka sasa kwa ajili ya suala hilo.
Ameahidi kuongeza mashine za kutosha kwa ajili ya usajili wa vitambulisho hivyo.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi, Eliud Leonard ameiomba serikali kuongeza muda wa usajili wa vitambulisho hivyo kutokana na kuwa mdogo huku wilaya hiyo ikiwa na watumishi wengi na mashine hizo zimekuwa zikisajili watu 150 katika vituo vya Misungwi na Usagara.
Eliud amesema wilaya yake ina vitongoji 723, vijiji 113, kata 27 na tarafa nne, hivyo imekuwa vigumu kufika sehemu za vijijini kutokana na uhaba wa usafiri.
Amesema wilayani hapo hadi sasa kuna walimu wa elimu ya msingi 511 huku 37 wakiwa hawajahakikiwa na walimu 37 wana vyeti vyenye utata. Watumishi wa Afya waliohakikiwa ni 525 ambapo watumishi 15 hawajahakikiwa na watumishi 66 wana vyeti feki.
Ofisa Msajili katika mkoa huo, Daudi Hashim amesema usajili wa vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa umma unaendelea na mpaka sasa wamesajili 10,634 wakiwamo walimu.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

DAR ES SALAAM
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema inatambua na itaendelea kuhakikisha watu wenye ulemavu wasio na uwezo wa kugharimia huduma za matibabu wanapatiwa msamaha wa matibabu katika ngazi zote kuanzia zahanati, vituo vya afya, hospitali za mikoa na za rufaa.

VAILETH JAILO

Aidha imesema kwa kutambua umuhimu wa huduma ya afya kwa wananchi wote, serikali kupitia wizara hiyo ipo katika mchakato wa kutungwa kwa sheria itakayowezesha wananchi wote wakiwemo watu wenye ulemavu kupata kitambulisho cha bima ya afya.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameyasema hayo katika tamko lake kuhusu huduma za matibabu kwa walemavu wasio na uwezo na kusema hatua hiyo itawaondolea vikwazo, wananchi wote wakiwemo watu wenye ulemavu katika kuzifikia huduma za afya pasipo kikwazo cha ukosefu wa fedha.
Amesema kutokana na maelezo hayo, Sera ya Afya ya Mwaka 2007 inatambua kuwa wapo wananchi wanakabiliwa na matatizo mbalimbali katika kuzifikia huduma za afya wakiwemo watu wenye ulemavu.
Ummy amesema kuwa Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Namba 9 ya mwaka 2010, pamoja na mambo mengine, inabainisha kuwa watu wenye ulemavu wana haki ya kuondolewa vikwazo katika kupata huduma za afya.
Pia amesema serikali itaendelea kusimamia na kuhakikisha makundi maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu ambao hawana uwezo wa kuchangia huduma za matibabu wanapata msamaha wa matibabu katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
 Ni marufuku kwa mtumishi yeyote wa sekta ya afya kuonesha vitendo vyovyote vya unyanyapaa na unyanyasaji kwa watu wenye ulemavu wanaofika katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Amesema mtumishi atakayethibitika kuonesha kwenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma na taaluma za afya kwa kufanya vitendo vya unyanyapaa na unyanyasaji kwa makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MOROGORO

KUSHAMIRI kwa ngoma za vigodoro katika wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro kumechangia kuwapo kwa mimba nyingi za utotoni ambazo ni tishio kwa maendeleo kielimu na kijamii.
VAILETH JAILO
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, amesema hayo, alipokuwa akielezea changamoto zinazoikabili wilaya hiyo mbele ya Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan, aliposimama kwa muda mjini hapo na kuzungumza na wananchi akiwa njiani kwenda Dodoma.
Mchembe, alisema mimba za utotoni katika wilaya hiyo zipo katika kiwango cha juu, zinachangiwa na ngoma za vigodoro, hivyo kuwafanya watoto wengi wa kike kukatisha masomo yao kutokana na kupata mimba na wengine kuzaa wakiwa na katika umri mdogo.
Hivyo alimwomba Makamu wa Rais, kutokana na fursa iliyopatikana na kuwepo kwake katika mji huo, azungumze na wazazi waliofika kumpokea kuhusu madhara ya mimba za utotoni.
Makamu wa Rais, amesikitishwa kuona watoto wadogo wa kike wanapata mimba wakiwa chini ya uangalizi na uzimamizi wa wazazi na walezi.
Hivyo alisema, kushamiri kwa mimba hizo za utotoni kunachangiwa na wazazi na walezi kushindwa kuwajibika ipasavyo katika malezi ya familia jambo ambalo linahatarisha maisha ya kielimu ya watoto hao.
Amesema, Serikali imeondoa ada kuanzia elimu ya awali, darasa la kwanza hadi kidato cha nne, ili kutoa fursa kwa watoto wote waweze kusoma bila vikwazo.
Hivyo, jukumu la wazazi na walezi ni kusimamia kwa karibu malezi ya watoto wao hasa wa kike ili wapate fursa ya kusoma kuanzia elimu ya awali hadi ya juu.
Makamu wa Rais, aliwataka wanafunzi wa kike kuzingatia falsafa ya uvaaji wa magauni manne ambayo ni sare ya shule, joho la mahafali, sare ya harusi na vazi la ujauzito na si kurukia vazi la ujauzito.
Ameagiza wazazi na walezi kuhakikisha mimba za utotoni katika wilaya hiyo, zinaondoka na kukomeshwa kabisa.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema anatamani wakuu wa wilaya za mkoa wa Dodoma wasihamishiwe maeneo mengine hadi pale azma ya serikali kuhamia Dodoma itakapokamilika kutokana na kufanya kazi kama timu.
EDITH PETER
Amesema hayo wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya wananchi wa mkoani Dodoma. Rugimbana alisema wakuu wa wilaya wamekuwa wakifanya kazi nzuri kwa kushirikiana na wakurugenzi.
Amesema mkoa wa Dodoma isingekuwa rahisi kutekeleza maamuzi bila Rais John Magufuli kukubali kuibeba Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Antony Mavunde amesema wananchi wa mkoa wa Dodoma wako tayari kuipokea serikali kuhamia Dodoma, kwani italeta mapinduzi makubwa katika biashara na hali ya uchumi.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
KIMATAIFA

CHINA
Afisa wa zamani wa ngazi ya juu nchini China, aliyepatikana ameficha dola za Kimarekani 30 milioni nyumbani mwake, amehukumiwa kunyongwa.
Hukumu hiyo hata hivyo imeahirishwa.
Wei Pengyuan alikuwa afisa mkuu aliyesimamia biashara ya makaa yam awe nchini China.
Mahakama katika mji wa Baoding, kaskazini mwa Uchina, imesema Bw Wei alipokea rushwa alipokuwa akiidhinisha miradi ya makaa yam awe.
Maafisa wa serikali wanasema mashine nne za kuhesabu pesa ziliharibika walipokuwa wanajaribu kuhesabu pesa zilizopatikana nyumbani kwa afisa huyo.
Maelfu ya maafisa wa serikali wameadhibiwa kwenye kampeni kubwa ya kukabiliana na ulaji rushwa nchini China.
Kampeni hiyo ambayo inaungwa mkono na Rais Xi Jinping imepelekea kuadhibishwa kwa baadhi ya wapinzani wa kisiasa wa Rais Xi.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

MAREKANI
Afisi moja ya chama cha Republican katika jimbo la North Carolina imeharibiwa na moto huku jengo lililo karibu yake likipakwa rangi ya nembo inayopinga chama cha Republican,mamlaka imesema.
Chupa iliojazwa mafuta yanayoweza kushika moto ilirushwa katika dirisha la makao makuu ya chama cha Republican kaunti ya Orange,chama hicho kimesema.
Mkurugenzi wa chama cha Republican, Dallas Woodhouse alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa,na kwamba tahadhari ya kiusalama imetumwa katika afisi nyengine za chama hicho.
Mgombea wa Democrat Hillary Clinton ameandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba shambulio hilo ni ''la kutisha na halitakubalika''.
Lakini Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump alionekana akiwalaumu wafuasi wa chama cha Democrat kwa kutekeleza kitendo hicho.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
CHINA
China imerusha roketi ambayo inawabeba wana anga wawili ambao wataenda kwenye kituo chake cha anga za juu kinachozunguka kwenye mzingo wa dunia.
Wana anga hao waliondoka kutoka chumba cha kurushia roketi na satelaiti cha Jiuquan kaskazini mwa Uchina.
Watatua katika kituo cha anga za juu cha Tiangong 2 ambapo watakaa siku 30, hicho kikiwa kipindi kirefu zaidi ambacho wana anga wa China wamekaa katika anga za juu.
Uzinduzi huo na miradi mingine iliyozinduliwa awali ni ishara za kujiandaa kwao kutuma watu Mwezini au katika sayari ya Mars.
Kituo cha awali cha anga za juu kilichoitwa Tiangong, Kasri la Mbinguni, kilifungwa mapema mwaka huu baada ya kupokea roketi tatu.
Wana anga walio kwenye roketi iliyorushwa sasa ni Jing Haipeng, 49, ambaye amewahi kwenda anga za juu awali mara mbili, na Chen Dong, 37.
Roketi hiyo ya Long March-2F imebeba chombo cha anga za juu kilichopewa jina Shenzhou-11, na ilipaa mwendo wa saa 23:30 GMT Jumatatu.
Wana anga hao watakaa kwa muda wakifanya utafiti kwenye kituo cha Tiangong 2.
Rais Xi Jinping akiwapongeza wana anga hao, amesema anatumai ufanisi huo "utaendeleza sana moyo wa usafiri wa anga za juu".
China imewekeza sana katika safari za anga za juu na inapanga kurusha roketi karibu 20 mwaka huu.
China ndiyo nchi ya tatu, baada ya Urusi na Marekani, kutuma binadamu anga za juu kwa kutumia watu kwa kutumia roketi zake binafsi.
China ilizuiwa kutumia Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) kutokana na dhana kwamba mpango wake wa anga za juu pia unakusudia kujiimarisha kijeshi.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment