MWANAFUNZI APIGWA NA WAALIMU SITA MPAKA KULAZWA

SIKU chache baada ya kutokea tukio la kushambuliwa mwanafunzi
ikiwa kama adhabu mkoani Mbeya katika shule ya Sekondari Kutwa ya Mbeya,
waalimu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe baada ya kudaiwa
kumshambulia mwanafunzi wa kike wa kidato cha nne kwa kosa la kukutwa na simu ya
mkononi katika begi lake la chuma (Tranka) la nguo na waalimu wake.
Mwanafunzi huyo wa shule ya binafsi ya sekondari ya Mbogamo,
ya mkoani Njombe, Elizabeth Simfukwe inadaiwa kushambuliwa na mkuu wa shule
akiwa na waalimu wengine na kumsababishia maumivu kisha kulazwa katika
Hospitali ya Kibena mkoani Njombe kwa siku zaidi ya tatu akipatiwa matibabu.
Nipashe imefika katika Hospitali ya Kibena inazuiliwa kumuona
mwanafunzi huyo na kuwa bado anapatiwa matibabu na anaendelea vizruri huku
akiwa amelazwa hapo kwa zaidi ya siku tatu tangu Oktoba 6 mwaka huu alipo
patiwa kipigo hicho.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Selina Nyoni, anasema kuwa
kweli mtoto huyo amelazwa katika Hospitali hiyo lakini kuna maelezo kutoka juu
hairuhusiwi kuonana na mtu yoyote kwa kuwa mtoto hiyo hajafa.
“Mtoto huyu amelaza hapa siku ya tatu anaendelea vizuri
lakini kuna maelezo nimepata hairuhusiwi mtu yeyote kumona na hairuhusiwi
habari zake kutolewa kwa kuwa jamo hili lina gusa jamii na huyu ni mtoto,”
alisema Dr Nyoni.
Kwa mujibu wa Dr Nyoni anasema kuwa mwanafunzi huyo aliletwa
hapo baada ya kupigwa na waalimu wake kwa viboko baada ya kukutwa na simu ya
mkononi ambapo inadaiwa kuwa alikuwa hataki kueleza anawasiliana na nani
kupitia simu hiyo ndipo waalimu wakaanza kumuazibu kwa viboko.
Mwanafunzi Elizabeth (19) wa kidato cha nne chanzo cha kupigw
ana waalimu 6 kwa kuchangiana inadaiwa ulipita ukaguzi shuuleni hapo na
kupatikana na simu kwenye begi lake ikiwa imezimwa kitu ambacho ni kosa.
Hata hivyo katika hospitalini hapo Nipashe inakutana na mtu
anaye daiwa ni kaimu afisa elimu ambaye anakana kuwa ni afisa elimu, na kuwa
anafanyia idara hiyo na Hospitalini hapo yupo kwaajili ya kuw ana mgonjwa wake.
Afisa huyo Anton inadaiwa kuwa ni kaimu afisa elimu alisema
kuwa Ofisini kwake kuhusiana na tukio hilo, taarifa hana uhakika kama imefika
licha ya yeye kuwepo ofisini.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri anakili kuwapo kwa
tukio hilo wilayani kwake licha ya yeye kuwa mbali ofisi ambapo anasema kuwa
alifika katika hospitali hiyo na kumuona na alimuona  mwanafunzi huyo  akiwa amepigwa na alama za fimbo.
Baadhi ya viongozi waliofika hospitalini hapo na kuzungumza
na mwanafunzi huyo wanaeleza hali yake ambapo bada ya kuzungumza na mwanafunzi
huyo walieleza kuwa alichapwa na waalimu baada ya kukutwa simu ya mkononikatika
begi lake.
Aidha diwani wa kata ya Ramadhani George Sanga anasema kuwa
mtoto huyo aliwaeleza kuwa alichangiwa na waalimu sita akiwemo na mkuu wa shule
hiyo.
Alisema kuwa mwanafunzi kuadhibiwa akiwa na kosa si tatizo
ila tatizo ni waalimu walivyo mwadhibu mwanafunzi huyo kwa kuwa kuwa na simu
hairuhusiwi kwa mwanafunzi.
Naye diwanai wa kata ya Mjimwema Abuu Mtamike alisema kuwa
kinacho msikitisha ni waalimu kumchangia mwanafunzi mmoja wakike huku waalimu
hao wengi wao wakiwa ni wanaume wakati shuleni hapo kulikuwa na mwalimu wa
kike.
Hata hivyo baba wa mtoto huyo alisema kuwa taarifa za bindiye
kupigwa alizipata kutoka kwa mtoto wake na kufika hospitalini kutoka mkoani
Songwe licha ya kuwa wakati akizungumza na Nipashe bado chanzo cha kupigwa kwa
mtoto wake alikuwa bado hajakijua.

from Blogger http://ift.tt/2dLwRtn
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment