Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo Mwishoni mwa wiki jana.
Mmoja wa wandiwani wa halmashauri a Mufindi akinena jambo katika baraza la madiwani halmashauri hiyo
MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa kwa wananchi wao juu ya kuwapo kwa mvua chache na kuwahimiza kupanda mazao yanayo stawi katika mvua chache.
Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa halmashauri hiyo imeshauriwa na wataalam kuhakikisha kuwa wanawataarifu wananchi kuwa mwaka huu kutakuwa na mvua chache kuliko kawaida.
Akitoa taarifa a Dharula mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya a Mufindi Festo Mgina alisema kuwa halmashauri hiyo kwa mwaka huu kutakuwa na mvua zisizo toshereli kwa kilimo cha kawaida na kuwa wananchi wake wanatakiwa kulima kwa kutumia megu zinazo komaa haraka na kulima mazao yanayo vumilia ukame.
Alisema kuwa madiwani hao wahakikishe kuwa kila mkutano wao wa hadhara na katika misiba mbalimbali watakayo shiriki wahakikishe kuwa wanatoa taarifa kwa wananchi ili waelewa taarifa hii na kujikinga na adha ya ukame na kukosa mavuno ya kutosha.
Alisema kuwa tahadhari hiyo imetolewa na wataaramu kutoka mamlaka ya hali ya hewa ambapo kwa msimu huu wa kilimo mvua zitakuwa ni chache.
Mgina anaomba maafisa ugani kushirikiana na madiwani kuwapa taarifa mara kwa mala kila mabadiliko yanapo tokea ili wananchi nao wafikiwe na taarifa hizo muhimu ili kuto ingia hasara.
Hayo yanaibuka katika mkutano wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Mufindi na kukaibuka kwa changamoto ya kuwapo kwa mapato kidogo ambapo madiwani wanaomba halmashauri kubuni mbinu mbalimbali za kuingiza mapato.
Madiwani hao wanasema kuwa ili kupandisha mapato huduma za afa ya jamii CHF kufana mafunzo kwa madiwani hao jinsi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge na halmashauri hiyo kuongeza mapato kutokana na mapato hayo.
Hata hivyo halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya asilimia 17 ya maelengo yake kwa muda wa miezi mitatu ya mwaka huu wa serikali ambapo kumekuwa na changamoto ya wakwepa mapato.
Mwisho
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi wakifuatilia jamo katika makabrasha yao kwenye mkutano wa Baraza la madiwani mwishi wa wiki jana, (Picha na Furaha Eliab, Iringa)
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza Kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Festo Mgina, (Katikati) katika kikao cha Baraza la kawaida la madiwani. (Picha na Furaha Eliab, Mufindi)
from Blogger http://ift.tt/2eIqSUq
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment