Leo
October 27, 2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kupitia kwa Waziri mwenye dhamana Ummy Mwalimu, imetoa tamko
kuhusu huduma kwa makundi maalumu na yaliyoko hatari zaidi kuambukizwa
na kuambukiza Virusi vya UKIMWI nchini Tanzania.
Waziri wa
Afya Ummy Mwalimu amesema kwa mujibu wa Takwimu za Viashiria vya UKIMWI
na Malaria za mwaka 2011-2012, kiwango cha maambukizi ya VVU nchini
kinakadiriwa kuwa ni asilimia 5.1 kwa watu wenye umri kati ya miaka 15 –
49. Takwimu hizi pia zinaashiria kwamba, kwa kila watanzania 1000, watu
51 miongoni mwao wanaoishi na maambukizi ya VVU.
Inakadiriwa kuwa, kuna watu 1,400,000 wanaishi na VVU nchini Tanzania ambapo, watu 839,574 wanapatiwa tiba ya dawa za kupunguza makali ya VVU zinazotolewa katika vituo 4,000 vilikuwa vinatoa huduma hiyo nchi nzima hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu (2016).
Inakadiriwa kuwa, kuna watu 1,400,000 wanaishi na VVU nchini Tanzania ambapo, watu 839,574 wanapatiwa tiba ya dawa za kupunguza makali ya VVU zinazotolewa katika vituo 4,000 vilikuwa vinatoa huduma hiyo nchi nzima hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu (2016).
Waziri
Ummy amesema kutokana na mazingira ya Tanzania, imeonesha kuwa makundi
maalumu ni makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukiza na
kuambukizwa VVU, kwa kuzingatia takwimu za maambukizi ya VVU kwa makundi
haya kuwa juu, huku Serikali ikiyataja makundi 13.
- 1. Wasichana walio katika umri wa balehe walio katika mazingira hatarishi.
2. Vijana walio katika umri wa balehe.
3. Watoto yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi (yaani watoto wanaoishi mitaani).
4. Wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao.
5. Wanawake wanaofanya ngono kinyume na maumbile.
6. Watu wanaotumia dawa za kulevya hasa wale wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano.
7. Wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wateja wao.
8. Wafungwa.
9. Wakimbizi na wafanyakazi wanao hamahama hasa madereva wa malori ya masafa marefu.
10. Wachimba madini na jamii zilizopo katika maeneo ya migodi.
11. Wavuvi na jamii zilizopo katika maeneo ya uvuvi.
12. Wafanyakazi wa kwenye mashamba makubwa.
13. Wajenzi wa barabara na watu wenye ulemevu.
Kuna
ushahidi wa kipiedemilojia kwa programu za VVU na UKIMWI kulenga makundi
maalum. Katika nchi zilizo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, vijana
balehe wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wanachangia asilimia 35 ya
maambukizi mapya ya VVU.
Aidha,
kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU nchini Tanzania, kinaonekana
miongoni mwa makundi maalum (asilimia 26 miongoni mwa Wanawake
wanaofanya Biashara ya Ngono, asilimia 36 miongoni mwa wanaotumia madawa
ya kulevya kwa kujidunga sindano na asilimia 25 miongoni mwa wanaume
wanaofanya ngono na wanaume wenzao).
0 maoni:
Post a Comment