DONALD TRUMP NA USALAMA WA UTAWALA HARAMU WA ISRAEL.

Siku tatu baada ya Donald Trump kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais wa Marekani, kumetolewa kauli kadhaa kuhusu namna Trump anavyoutazama usalama wa Israel.
Danny Danon Balozi wa Utawala wa Kizayuni wa Israel katika Umoja wa Mataifa amesema rais mteule wa Marekani pamoja na wapambe wake ambao anajuana nao kwa muda mrefu, wanafungamana na suala la kudhamini usalama wa Israel.
Baada ya kuchaguliwa Trump, na kwa kuzingatia kuwa amesema atazingatia zaidi masuala ya matatizo ya ndani ya Marekani, swali linaloulizwa ni hili kuwa, je, Trump atautazama vipi uhusiano na utawala wa Israel na hasa usalama wa utawala huo?
Israel ni muitifaki mhuimu zaidi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati. Ushawishi wa Lobi ya Kiyahudi nchini Marekani ni mkubwa kiasi kwamba kila  ambaye anachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, hushawishiwa pakuba na lobi hiyo.
Ingawa serikali ya  Barack Obama ilifungamana na sera ya kudhamini usalama wa Israel lakini rais huyo anayeondoka alihitilafiana sana na Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala huo wa Kizayuni.
Vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel
Wakuu wa Israel walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mapatano ya nyuklia baina ya Iran na madola sita makubwa duniani ya kundi la  5+1 ambapo Marekani ilikuwa na nafasi kubwa katika kufikiwa mapatano hayo.
Inaelekea kuwa, serikali yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia Israel imeridhika na kuchaguliwa rais kutoka chama cha Republican nchini Marekani.
Masaa machache baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais Marekani, Trump alizungumza kwa simu na Netanyahu na kumfahamisha kuwa atakutana naye katika 'fursa ya kwanza'.
Kwa mujibu wa matamshi yaliyotolewa na watu mbali mbali, inaelekea kuwa Trump, sawa na marais waliomtangualia, atafungamana kikamilifu na sera ya kudhamini usalama wa Israel.
Danny Danon aliwahi kukutana na Trump miaka kadhaa hata kabla hajajitosa kwenye siasa na hivyo amesema hakuna haja ya kuwepo wasi wasi kuhusu uhusiano wa Israel na Marekani baada ya kuchaguliwa Trump. Ameongeza kuwa, uhusiano wa Marekani na Israel ni wa kina sana na kwamba hakuna shaka kuwa Trump na timu yake katika Ikulu ya White House ni marafiki wa Israel.
Jason Dov Greenblatt, Yahudi mwenye misimamo mikali, ni kati ya washauri wa ngazi za juu wa Donald Trump na amenukuliwa akisema kuwa, "Trump amesema hatua ya Israel kujenga vitongoji vya walowezi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu 'si kizingiti kwa amani' na hivyo haipaswi kulaaniwa"
Danny Dannon Balozi wa Utawala haramu wa Israel katika Umoja wa Mataifa
Greenblatt ametoa kauli hiyo katika hali ambayo serikali ya Obama imekuwa ikisema wazi kuwa, hatua ya Israel kujenga vitongoji katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni chanzo kikuu katika kuvuruga kile kinachodaiwa kuwa ni mchakato wa amani baina ya Israel na Palestina.
Naye Naftali Bennett waziri wa elimu katika utawala wa Israel ambaye ni mwanachama wa chama chenye misimamo mikali cha Yisrael Beiteinu (Israel ni Nyumba ya Mayahudi) ametoa kauli muhimu na kusema anaamini kwamba kwa kuchaguliwa Trump suala la kuundwa nchi huru ya Palestina sasa halipo tena na limepitwa na wakati.
Ingawa kauli ya Bennet ni ya kufurutu ada lakini ushahidi unaonyeshoa kuwa katika zama za urais wa Trump uhusiano wa Israel na Marekani utakuwa wa karibu zaidi kuliko wakati wa Obama.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment