Ndege za kijeshi za Saudia zimeendelea kufanya mashambulio ya anga
katika maeneo mbalimbali ya Yemen na kuzidi kusababisha uharibifu mkubwa
na mauaji dhidi ya raia wasio na hatia yoyote wakiwemo wanawake na
watoto wadogo.
Kanali ya Televisheni ya
al-Mayadeen ya Lebanon imetangaza kuwa, ndege za kijeshi za Saudia
zimeshambulia kwa mabomu maeneo kadhaa ya magharibi mwa Yemen na
kupelekea kwa akali watu watatu kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Ripoti zinaeleza kuwa, miji ya Sa'adah
na Sana'a ambao ndio mji mkuu wa Yemen ni miongoni mwa maeneo ambayo
yameendelea kushambuliwa kwa mabomu na ndege za kijeshi za Saudi Arabia.
Wakati huo huo, wanajeshi 8 vamizi wa
Saudia wameangamizwa katika mji wa Taiz baada ya kushambuliwa na vikosi
vya kujitolea vya wananchi.
Mashambulio hayo ya kinyama ya Saudia
hadi sasa yameshaua zaidi ya Wayemeni elfu kumi, kujeruhi mamia ya
maelfu ya wengine au kuwaacha bila ya makazi mbali na kuteketeza
asilimia 80 ya taasisi za miundombinu na za utoaji huduma na tiba za
nchi hiyo masikini ya Kiarabu.
0 maoni:
Post a Comment