MBEYA
Jeshi la
polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa mbeya kimewataka wamiliki wa
vyombo vya usafiri kuajiri madereva wenye leseni halali ili kupunguza usumbufu
wa vyombo hivyo kutokutembea barabarani.
Hayo
yamesemwa na kamanda kamishna wa kikosi cha usalama barabarani wa mkoani mbeya
BUTUSYO MWAMBELO wakati wa akizungumza na waandishi wa habari waliotaka
kujua kuhusu madereva wasio na leseni
wala kibali chochote ili mradi mliki anamtambua.
Butusyo
ametaka halmashauri jiji kushirikiana
kwa pamoja ili kuondoa vibanda vilivyopo kando kando mwa stand kutolewa kwani
wamekuwa wakiwauzia madereva,makondakta pamoja na wapiga debe vilevi na
kusabisha athari ndani ya jamii.
Aidha
BUTUSYO amesema kuanzia tarehe disemba mosi mwaka huu watafanya oparesheni kali
itakayofanyika kwa wote wasio na leseni na hawaruhu dereva yeyote asiye na
leseni kuingiza usafiri wake barabarani.
Kwa upande
wake kamanda wa polisi mkoa wa mbeya DHAHIRI KIDAVASHARI amesema kuwa
haitaruhusiwa mtu yeyote kuendesha chombo cha moto pindi ifikapo tarehe mosi
mwaka huu.
Na kwa upande wao madereva wamekiri kuwa hii
ni changamoto kwao
0 maoni:
Post a Comment