LINDI
Wananchi wa
kijiji cha kibata kilichopo katika kata ya kibata wilayani kilwa mkoani lindi wameomba halmashauri ya
wilaya hiyo kuimarisha barabara za vijijini ili kurahisisha shughuli za
usafirishaji kwa kipindi chote cha mwaka .,
Wakizungumza
na waandishi wa habari wananchi hao wamesema wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto mbalimbali za usafiri wa barabara katika kipindi cha msimu wa mvua
za masika kutokana na hali duni ya miundo mbinu ya barabara inayounganisha
kijiji hicho katika kipindi cha mvua za masika na maeneo mengine ya wilaya ya
kilwa.
Hayo
yanajiri kufuatia gari ya mizigo aina ya kia yenye namba za usajiri T.396 ACQ
ikiwa imeanguka na kufunga njia huku bidhaa mbalimbali zikiwa zimesambaa huku
na huko ikiendeshwa na kaniso kilipo.
Kwa mujibu
wa mashuhuda ambao pia wametoa msaada katika ajali hiyo said abdallah na ally
mketo wamesema kuwa tatizo kubwa katika maeneo hayo ni miundombinu mibovu ya barabara hali inayoweza kusababisha
ajali zisizo za lazima.
Mbunge wa
kilwa kaskazini THE RASTO NGOMBALE
amesema kuwa wanaitumia barabara hiyo kwa kiasi kikubwa kutoka dare s salaam kwa kusafirisha mahitaji
mbalimbali lakini miundo mbinu yake hairidhishi hivyo wameiomba serikali
kuangalia namna ya kusaidia
Mkuu wa mkoa
wa lindi godfrey dhambi akiongozana na
mkurugenzi wa halmashauri ya kilwa zabron bugingo kaimu mkuu wa wilaya pamoja
na mhandisi na baadhi ya wakuu wa idara amesikiliza kero hizo za wananchi
ikiwemo barabara.
0 maoni:
Post a Comment