Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura amewataka wachezaji
wa mchezo wa kuogelea kuiwakilisha nchi vizuri katika mashindano ya
dunia yanayotarajiwa kuanza Desemba 6 mwaka huu nchini Canada.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akimkabidhi bendera Nahodha wa timu ya Taifa ya kuogelea Hilal Hilal
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi bendera kwa waogeleaji sita wanaotarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Canada, Waziri Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na michezo Annastazia Wambura amesema, bendera aliyowakabidhi haitakuwa na maana iwapo wataenda kujaribu na siyo kushindana kama walivyoahidi na ushindi watakaoupata siyo sifa ya kwao pekee bali ni ya taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake kocha wa mchezo huo John Belela amesema, amewaandaa vizuri wachezaji wake kwa ajili ya mashindano hayo yanayotarajiwa kushirikisha waogeleaji zaidi ya elfu moja kutoka nchi mbalimbali duniani na anaamini watashinda kwani wameshashiriki mashindano mbalimbali makubwa ambayo yamewapa mwanga wa kujua ni kitu gani wanatakiwa kufanya ili kushinda.
Msafara utakuwa na jumla ya watu 12 ambapo wachezaji watakuwa sita na viongozi sita.
Wachezaji watakaoondoka kesho kuelekea nchini Canada kushiriki mashindano hayo ni Hilal Hilal ambaye ni nahodha wa kikosi hicho, Adil Bharmal, Denis Mhili, Joseph Sumai, Catherin Mason na Sonia Samiotto.
0 maoni:
Post a Comment