Majambazi wavamia mgahawa, wapora na kujeruhi




Watu wanaodaiwa kuwa majambazi wamevamia mgahawa wa Dinners jijini Mwanza uliopo katika mtaa wa Kenyatta Road na  kupora kiasi cha fedha kisichojulikana na kujeruhi watu wawili kwa risasi kabla ya kutoweka.
Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo majambazi hao wanadaiwa kuingia ndani ya mgahawa huo majira ya alasiri na kufyatua risasi kadhaa kutoka ndani ya mgahawa huo.
Tukio hio limetokea katika eneo ambalo limezungukwa na taasisi za kibenki ikiwemo benki ya NMB, Kenya Commercial Bank KCB na wakala wa benki ya CRDB na zote zikilindwa na askari ambao hawakuweza kutoa msaada wowote licha ya kuwa ndani ya mita 30 kutoka katika mgahawa huo.
Moja ya watu waliojeruhiwa alikuwa ni muuza mitumba nje ya mgahawa huo  na mwingine akiwa na asili ya Asia ambaye haijajulikana alikuwa nani katika mgahawa huo.
Akizungumza katika tukio hilo Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema atazungumza na vyombo vya habari kesho  baada ya kupata taarifa kamili.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment