Meya wa mji wa
Clay, Jimbo la West Virginia nchini Marekani amejiuzulu, baada ya
kuhusika na taarifa za ubaguzi wa rangi dhidi ya Mke wa Rais Obama
Michelle Obama.
Beverly Whaling alionekana kuunga mkono taarifa
kwenye mtandao wa Facebook iliyomfananisha bi Obama na ''nyani
aliyevalia viatu'',. Meya huyo aliandika kwamba ujumbe huo
ulimfurahisa sana, lakini baadae akakanusha na kusema alimaanisha
alifurahia matokeo ya uchaguzi Mkuu.Kumekua na saini 170,000 kumtaka
meya huyo kuachia ngazi. Bi Whalling ni meya wa mji wa Clay ulio na
wakaazi 491 pekee asili mia 98 wakiwa wazungu. Image copyrightWHITE HOUSEImage caption
Melania Trump na Michelle Obama
Meya alichangia ujumbe uliowekwa na bi Pamela Ramsey
Taylor mkaazi wa mji huo aliyesema inaridhisha kuona kwamba ikulu ya
Rais sasa itakua na Mke wa Rais anayependeza na kwamba amechoshwa
kumuona ''nyani aliyevalia viatu'', akiwa ndani ya ikulu.
Licha ya
mji wa Clay kuwa na wakaazi wachache hata hivyo ujumbe huu wa Facebook
ulisambaa kote nchini na kuzua ghadhabu ya umma kwa kuwa wa kibaguzi. Bi
Taylor ameachishwa wadhifa wake kwenye shirika moja la kijamii mji wa
Clay. Meya ameomba radhi na kusema majibu yake siyo ya ubaguzi wa rangi.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment