PAUL MAKONDA ALIVYOAMURU MWENYEKITI MWINGINE AKAMATWE KATIKATI YA MKUTANO

 Paul Makonda alivyoamuru mwenyekiti mwingine akamatwe katikati ya mkutano


November 24 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salam, Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku 10 ambayo lengo ni kukutana na wanannchi kwa ajili ya kusikiliza kero zao. Ilikuwa ni zamu ya Ilala na hapa ulikuwa ni mkutano wa hadhara Chanika, katika mkutano huo ulitawaliwa na kero kubwa moja ambayo ni suala la ardhi.

Moja ya kero iliyowasilishwa ni kuhusu mwenyekiti wa mtaa wa Zavala ambaye anatuhumiwa kuuza ardhi kinyume cha sherialikiwemo eneo lililotengwa kwa ajili ya kuhamishia wananchi wa kata ya Kipawa ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege.

RC Makonda baada ya kuwasikiliza baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa waliotoa ushuhuda kuhusu tuhuma hizo aliamuru mwenyekiti kukamamtwa katikati ya mkutano. Unaweza kuangalia ilivyokuwa kwenye hii video hapa chini.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment