Siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu Marekani
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump na wa Democratic
Hillary Clinton wameimarisha kampeini zao leo katika mkondo wa mwisho wa
kampeni hizo, zikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya uchaguzi mkuu
nchini Marekani.
Clinton anategemea umahiri wake kumsaidia kushinda katika uchaguzi huo ambao uchunguzi wa maoni unamuonyesha anaongoza kwa asilimia 48 dhidi ya Trump anayeungwa mkono kwa asilimia 43.
Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha wagombea hao hawajaachana sana.Wanamuziki Beyonce na mumewe Jay Z walikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliojitokeza kumfanyia kampeni Clinton hapo jana.
Rais Barack Obama pia anatarajiwa kumfanyia kampeini za lala salama Clinton. Katika jimbo la Nevada, Trump alilazimika kuondolewa jukwaani na maafisa wa usalama kufuatia kitisho cha kushambuliwa kwa bunduki.
Hata hivyo maafisa wa usalama wamesema hakukupatikana silaha yoyote. Kambi ya Trump ina matumaini ya kuwashawishi wapiga kura zaidi kumuunga mkono mgombea wao katika uchaguzi huo wa Jumanne.

About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment