TAKWIMU MUHIMU KUELEKEA LONDON DERBY ARSENAL VS SPURS LEO




Arsenal leo wanakabiliwa na kibarua kigumu watakapokuwa maskani yao Emirates kuwakaribisha mahasimu wao Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Premier Legue utakaofanyika saa tisa alasiri kwa majira ya Afrika Mashariki.

Timu zote zinaingia katika mchezo wa leo zikiwa na rekodi tofauti tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi mwezi August mwaka huu.

 

Dondoo muhimu kuelekea mchezo wa mahasimu hawa
  • Tottenham wameshinda mara moja kwenye dimba la Arsenal ndani ya mechi 26 walizokutana kwenye michuano yote tangu Mei 1993 (sare 10, kufungwa mra 15).
  • Ushindi huo ulikuwa ni ule wa 3-2 waliopata Novemba 2010, wakati walipotoka nyuma kwa mabao 2-0 kipindi cha kwanza na kufanya maajabu kipindi cha pili.
  • Arsenal hawajapata ushindi mbele ya Spurs kwenye michezo minne ya Premier League iliyopita (sare 3, kufungwa mara moja), na hawajawahi kucheza michezo zaidi ya mitano bila kupata ushindi dhidi ya mahasimu wao hao chini ya utawala wa Arsene Wenger. Hata hivyo waliwafungwa Spurs katika mchezo wa Kombe la Ligi msimu uliopita.
  • Mauricio Pochettino hajafungwa kwenye michezo minne dhidi ya Arsenal tangu alipowasili White Hart Lane. Hakuna kocha mwingine yeyote wa Spurs ambaye amewahi kufanya hivyo dhidi ya Arsenal.
  • Katika pambano la mahasimu hawa, timu inayotangulia kufunga imeshindwa kushinda mchezo kwenye matukio 23, idadi kubwa zaidi kwenye historia ya Premier League (sare 15, vipigo mara nane).
  • Mchezo pekee wa mahasimu hawa wa Premier Leage ulochezwa mchana ulikuwa ni ule wa Novemba 2004, Arsenal walishinda mabao 5-4 katika Uwanja wa White Hart Lane.
Arsenal
  • Arsenal wameshinda mechi 10 kati ya 11 zilizopita kwenye michezo ya ligi na Kombe la Ligi, wakifunga jumla ya mabao 32.
  • Wamepoteza mchezo mmoja tu wa Premier League lati ya 20 iliyopita (wameshinda 12, sare mara 7).
  • Mesut Ozil amehusika moja kwa moja kwenye mabao 8 katika michezo mitano iliyopita kwa upande wa Arsenal kwenye michuano yote (amefunga mabao matano, na kutoa assist tatu).
Tottenham Hotspur
  • Tottenham hawajafungwa kwenye mechi 10 za mwanzo za ligi kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1990-91.
  • Wasipofungwa leo maana yake watakuwa wamecheza mechi 11 za awali bila ya kupoteza kwenye Ligi ya Premier kwa mara ya tatu baada ya 1960-60 (michezo 16) na 1959-60 (michezo 12). Katika misimu yote hiyo walimaliza katika nafasi za kwanza na tatu mtawalia (licha kwamba wakati huo ushindi ulihesabiwa kwa poiti mbili).
  • Spurs wana rekodi nzuri ya safu ya ulinzi kwa sasa kwenye Premier League, wakirhusu mabao matano tu mpaka sasa.
  • Endapo watatoka sare leo, itakuwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tangu Aprili 2008.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment