TAKWIMU HII INAZIDI KUMSAULISHA KABISA MOURINHO MBELE YA MASHABIKI WA CHELSEA NA CONTE BKUZIDI KUTUKUZWA.



Antonio Conte amekuja msimu huu Chelsea na ghafla amegeuka kuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo kutokana na mfululizo wa matokeo mazuri kwenye Ligi ya England ukilinganisha na hali iliyokuwa msimu uliopita chini ya Chelsea.
Baada ya vipigo viwili vya aibu kutoka kwa Liverpool na Arsenal, Muitaliano huyo aliamua kubadili mfumo na kutumia mfumo wa 3-4-3 na kufanya mambo mazito sana klabuni hapo ndani ya muda mfupi sana.
1
Tangu aanze kutumia mfumo huo, Chelsea imeshinda michezo yote mitano, imefunga mabao 16 bila kuruhusu nyavu zao kutikishwa hata mara moja.
Inawezekana mashabiki wengi wa Chelsea walisikitishwa na kitendo cha mmiliki wao kumtimua Mourinho msimu uliopita, lakini kwa sasa wanmeanza kusahau baada ya mfululizo wa matokeo mazuri na kutoa vipigo vizito kwa wapinzani wao wakiwemo Man United chini ya Mourinho waliokufa 4-0 Darajani.
Kitu cha ajabu zaidi ni takwimu kuonesha kwamba tangu kuanza kwa msimu mpya, Conte ameshinda michezo ya mingi zaidi ya Premier League dhidi ya Mourinho ikijumlishwa michezo ya msimu uliopita na huu wa sasa.
Chelsea wameshinda michezo nane mpaka sasa chini ya Conte wakiwa kileleni, wakati Manchester United chini ya Mourinho wameshinda michezo minne tu ukijumlisha na ile minne ya msimu uliopita alipokuwa akiifundisha Chelsea jumla inakuwa nane.
Licha ya United kumpa Mourinho fedha nyingi zaidi kwenye usajili msimu huu kuliko Conte na Chelsea yake, lakini Conte amejikutana akipata mteremko zaidi na kuifanya Chelsea kuwa timu zinazopewa kipaumbele katika mbio za ubingwa mpaka sasa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment