WAANGALIZI WA KIGENI KUFUATILIA UCHAGUZI WA MAREKANI.


Waangalizi wa uchaguzi wanatizama kura zikihesabiwa Novemba 2014 katika uchaguzi wa wajumbe wa Senate huko Juneau, Alaska.

Waangalizi wa uchaguzi wanatizama kura zikihesabiwa Novemba 2014 katika uchaguzi wa wajumbe wa Senate huko Juneau, Alaska.

Wakati wapiga kura wakielekea kwenye vituo vya kupigia kote nchini Marekani Jumanne Novemba 8 mamia ya waangalizi wa kigeni watakuwa wanafuatilia uchaguzi wa rais mpya na wabunge.

Waangalizi wanawakilisha taasisi mbili kubwa ambazo kwa muda mrefu zina historia ya kazi kama hii, lakini zinajulikana sana ya kufanya kazi hiyo katika maeneo mengine ya dunia na siyo Marekani.

Serikali ya Marekani imeiomba taasisi ya mataifa ya Amerika yenye makao yake si mbali na ikulu ya Marekani kufuatilia kwa mara ya kwanza uchaguzi wa mwaka huu.

“Marekani inaiheshimu kazi kubwa ya OAS ya kuhamasisha chaguzi huru na za haki kote katika eneo hili", amesema mwakilishi wa Marekani katika OAS, Kevin Sullivan. "Tunakaribisha uangilizi wa OAS kama fursa ya kuonyesha nia ya dhati ya Marekani kuunga mkono kazi muhimu sana ya taasisi hii.’

Aliyekuwa rais wa Costa Rica, Laura Chinchilla anaongoza juhudi hizo kwa kuhusisha takriban watalaamu 40 kutoka mataifa 16.

Taasisi ya usalama na ushirikiano huko barani ulaya (OSCE), ambayo ilifuatilia uchaguzi wa mwaka 2012 na wengine sita hapa Marekani wanarejea kwa uchaguzi wa mwaka huu.

Taasisi hiyo yenye mataifa wanachama 57 ina timu kubwa kuliko OAS, yenye zaidi ya waangalizi 600 kwa jumla. Wengi wamelenga katika kufuatilia taratibu kwenye vituo vya kupigia kura, wakati baadhi wakiangalia picha kubwa ya utaratibu wa uchaguzi katika kiwango cha majimbo.

Timu za kimataifa zitafanya kazi sambamba na wanaofuatilia upigaji kura kutoka vyama vya siasa, jukumu ambalo limepata umaarufu wakati wa kampeni za urais huku mgombea wa Republican Donald Trump akielezea wasi wasi wake kuhusu wizi wa kura.

OAS imesema nchini Marekani wataangalia masuala yanayohusisha maandalizi ya uchaguzi, teknolojia, fedha za kampeni na ushiriki wa kisiasa, na kutoa ripoti itakayoelezea taratibu mzuri na maboresho gani yanaweza kufanywa.

OSCE pia itatoa mapendekezo katika ripoti yake ambayo wataiwasilisha kwa serikali na kwa umma.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment