UAL YAPELEKA WANAFUNZI 50 CHINA KUSOMEA MASUALA YA PETROLI, GESI NA AFYA


Jumla ya vijana 50 wameondoka nchini leo kuelekea China, kusomea kozi mbalimbali ikiwemo za afya na uhandisi katika masuala ya Petroli kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza masomo yatakayochukua miaka minne na sita kutegemea na aina ya kozi.
Wakizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kupaa kuelekea China, vijana hao wameelezea matumaini yao kuwa stadi na maarifa wanakayokwenda kupata nchini humo katika Shahada za Udaktari na Upasuaji, Uhandisi wa Masuala ya Petroli na Usanifu Majengo, vitakuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Thomas Macha na Sabir Abdulrahman, wanaokwenda katika vyuo vikuu vya majimbo ya Shenyang na  Hubei, wamezungumzia matarajio yao, wakiamini masomo wanayoenda kusoma yataisaidia Serikali kuelekea Tanzania ya Viwanda inayohubiriwa na Serikali ya Wamu ya Tano.
Miongoni mwa wasichana 20 kati ya vijana hao 50 wanaokwenda nchini humo, Monica Malugu na Anastacia Meresho, nao wamezunguzia matarajio yao ikiwemo mitazamo kuwa wanawake hawawezi masomo fulani kwa kuwa ni magumu.
Aidha, Glory Minja, mwakilisi wa Taasisi ya Universal Abroad Link (UAL), yenye dhamana ya kuwatafutia vyuo na ushauri kulingana na soko la ajira na kujiajiri, amesema,kila kitu kiko sawa na kwamba wanasubiriwa kuanza masomo.
Meneja wa Taasisi ya Universities Abroad Link (UAL), Joash Hosea akiagana na baadhi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nchini China kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanafunzi 50 wamekwenda China kwa ajili ya masomo ya Udaktari, Uhandisi pamoja na Mafuta na Gesi
Esther Sanga (wa tatu kushoto) akiwa na familia yake muda mfupi kabla kupanda ndege kuelekea nchini China kwa masomo.
Wanafunzi wanaokwenda katika kusoma katika vyuo vikuu nchini China wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wao.
Wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vikuu nchini China wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wao.
Wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vikuu nchini China wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vikuu nchini China wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nchini China wakimsikiliza Meneja wa Taasisi ya Universities Abroad Link, Joash Hosea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya wanafunzi 50 walikwenda China kwa ajili ya masomo ya Udaktari, Uhandisi pamoja na Mafuta na Gesi

from Blogger http://ift.tt/2g8O13v
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment