Kijana wa Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akizungumza kwenye mkutano wa wakazi wa mtaa huo kujadili maagizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama kwenye ngazi ya Mtaa. Mkutano huo umefanyika Novemba 20, 2016
Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Bw.Kassim Mohammed Mnyoge, akizungumzia maagizo hayo
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAKAZI wa Mtaa wa Mbagala- Kiburugwa, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wamefanya kikao Jumapili Novemba 20, 2016, cha kujadili maagizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama ngazi ya Mtaa.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata Bw.Saleh Kaitani, alisema, kikao hicho kitajadili mambo mawili, mosi ni maagizo ya SACP Muroto na pili ni masuala ya mpango wa kusaidia kaya masikini wa TASAF.
Kusuhusu suala la ulinzi na usalama, Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa huo, Bw.Kassim Mohammed Mnyoge alisema, SACP Muroto katika kikao chake na watendaji kilichofanyika Oktoba 28, 2016 kwenye shule ya msingi Kigungi, alitoa maagizo kadhaa kuhusu hatua za kuchukua katika kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika suala la ulinzi na usala.
“Kila mjumbe wa mtaa kwa kushirikiana na Mratibu, waorodheshe katika daftari wakazi wa mtaa husika ili kujua idadi yao na shughuli wanazofanya.” Alisema Bw. Kassim wakati akiwasilisha taarifa kwa wananchi.
Mtaa wa Kiburugwa una wakazi wanaofikia 18,000 kwa mujibu wa Bw. Kassim.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo la Ulinzi na Usalama, Bw. Kassim alisema, SACP Muroto ameagiza wananchi mjadili jinsi ya kushiriki katuika suala la ulinzi na usalama kwenye mitaa.
Kila mwenye nyumba, anapotembelewa na mgeni ni lazima akatoe taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi au kwa mratibu wa eneo husika, lakini pia kila mwananchi lazima ashiriki kwenye suala la ulizni na akikaidi Mjumbe wa mtaa apelike taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ili taarifa hiyo imfikia RPC kwa hatua za kisheria ambazo adhabu zake ni faini ya shilingi elfu 50,000 au kifungo cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja.
Maagizo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja wazazi kuwadhibiti watoto wao, na endapo mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 atajihusisha na vitendo vya kihalifu kama kujiunga na makundi ya “panya road”, basi mzazi wa mtoto huyo atakamatwa kwa vile ni jukumu lake kuhakikisha mtoto huyo anakuwa katika maadili mema.
Wakichangia kwenye mjadala huo, wananchi wengi wamekubaliana na maagizo hayo ya kushiriki kwenye ulinzi lakini wakaonyesha wasiwasi namna ya utekelezaji wake.
“Ninapenda nijulishwe, ulinzi huu ambao wananchi tunatakiwa kushiriki ni wa namna gani, maana hali ya sasa sio kama ile ya zamani ya enzi za Mrema, mambo ya sungusungu kutembea na panga nataka kujua tunalindaje na usalama wetu ukoje endapo nitadhurika.” Aliuliza mwananchi mmoja Bw.Hamisi Omary Libinongi.
Mwananchi mwingine, alisema, ni vema wananchi wanapolinda wakaongozana na askari wenye silaha, kwani wahalifu wa sasa, wanabeba silaha nzito nzito na kwamba itakuwa hatari kwa mwananchi kufanya doria kwa kutumia panga pekee.
Akijibu hoja kuhusu jinsi ya ushiriki wa wananchi katika ulinzi, Mwneyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Bw.Said Mwinshehe Ng’agi, alisema, wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi katika suala hilo la ulinzi, kwani kila kundi la wananchi wanaolinda kwenye eneo fulani, wataongozana na askari wawili wenye silaha.
Naye Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata hiyo ya Kiburugwa, Bw.Salehe Kaitani, amesema maagizo hayo ni ya serikali na wananchi hawana buni kushirikiana ili kuyatekeleza. “Wananchi tunapaswa kutekeleza maagizo haya ya Jeshi la polisi, najua zipo changamoto za baadhi ya askari kutokuwa waaminifu, lakini kama mjuavyo askari wa namna hii ambao hawana wito, wamekuwa wakichukuliwa hatua na nyinyi wananchi toeni taarifa kwa viongozi kama mnakutana na askari wanaodai rushwa.” Alisema Bw. Laitani.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa huo, Bw.Said Mwinshehe Mng’agi, (kulia), akiwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Bw.Salehe Kaitani, akifafanua baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi
Mwananchi akiuliza swali kuhusu utaratibu wa kiulinzi kwa kushirikiana na wajumbe wa mtaa.
Mwananchi akiuliza nini umuhimu wa vijana wa ulinzi shirikishi kwenye mitaa
Mzee Hamisi Omary Libinongi, akkuliza namna wananchi watakavyotekeleza ulinzi huo bila ya kupatwa na madhara
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Bw.Salehe Kaitani, akifafanua baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi
Mjumbe wa nyumba kumi, Bw. Jumanne Mohammed Ngayeka almaarufu kama “Nongwa” aliuliza swali
from Blogger http://ift.tt/2fRZAcd
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment