Leo December 15 2016 mkuu wa mkoa wan Dar es salaam, Paul Makonda amefanya ziara katika soko la kariakoo ili kusikiliza na kujibu kero mbalimbali za wafanyabiashara wa soko hilo. Nimekuwekea hapa baadhi ya yaliyojiri kwenye ziara hiyo.
'Soko lilitengenezwa kwa ajili ya mazao lakini soko limebadilika linauza bidhaa za viwanda' ;-RC Makonda #DarMPYA#SokoKARIAKOO
'Viongozi wetu wanaosimamia soko wameonyesha namna soko linavyojiendesha bila kutengeneza faida' RC Makonda #DarMPYA#SokoKARIAKOO
'Sijaridhishwa na mwenendo wa watu wanaotuwakilisha kwenye soko la kariakoo'- RC Makonda #DarMPYA #SokoKARIAKOO
'Nataka uchunguzi ufanyike kujua vyanzo vyote vya mapato ya soko la kariakoo'- RC Makonda #DarMPYA #SokoKARIAKOO
'Naagiza ufanyike uhakiki inawezekana tukakuta watumishi hewa ndani ya soko la kariakoo' -RC Makonda #DarMPYA#SokoKARIKAOO
'Wafanyabiashara wanaohujumu maeneo kwa kuwa na vizimba zaidi ya 10 na kazi ni kukusanya kodi wajiandae kuviachia'-RC Makonda#SokoKARIAKOO
'Tunaunda uongozi wa mpito wa machinga DSM, tunataka umoja utakaoondoa adha na dhuluma'- RC Makonda #MtaawaCONGO#DarMPYA
0 maoni:
Post a Comment