China yapeleka kikosi cha tatu cha askari wa miguu wa kulinda amani Sudan Kusini


China imepeleka awamu ya kwanza ya askari 120 wa miguu kati ya 700 wa kikosi cha kulinda amani katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.
Walinda amani hao walipata mafunzo maalum ya miezi mitatu ya kulinda amani na watakuwa na majukumu ya kulinda raia, kusaidiana na Umoja wa Mataifa katika majukumu ya kulinda haki za binadamu na kufanya doria.
Kikosi hiki ni cha 3 kwenda Sudan Kusini tangu kikosi cha kwanza cha kulinda amani kupelekwa mwaka 2015. Mwezi Julai mwaka huu, askari wawili wa kulinda amani wa China waliuawa na watano kujeruhiwa wakati wa kulinda amani mjini Juba.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment