Liverpool walifunga Bao zao 2 za kwanza kupitia Sadio Mane na Divock Origi kabla Haftaimu na Bournemouth kupata Penati na kufunga Dakika ya 56.
Lakini Liverpool wakaongeza bao la 3 lililofungwa na la Emre Can.
Bournemouth wakapiga Bao lao la Pili kupitia Fraser Dakika ya 76 na Dakika 2 baadae Gemu kuwa 3-3 kwa Bao la Cook.
Bao la 4 na la ushindi Dakika ya 93 Mfungaji akiwa Nathan Ake.
Katika mchezo mwingine wa EPL, Manchester United yalazimishwa sare na Everton
Wenyeji Everton wamepata Sare ya 1-1 walipocheza na Manchester United huko Goodson Park kwenye Mechi ligi Kuu England- EPL kwa msaaada wa Penati ya Dakika ya 89 iliyotolewa na Refa Michael Oliver.
Man United walitangulia kufunga katika Dakika ya 42 kwa Bao safi la Zlatan Ibrahimovic alipomvisha kanzu Kipa Stekelnburg alietoka Golini kuufuata Mpira ambao uligonga Posti ya juu, ya pembeni na kisha kuvuka mstari huku Beki wa Everton akiuokoa lakini Bao hilo kuthibitishwa na mfumo wa Kielotriniki wa GLD, Goal Line Decision.
Katika dakika ya 89 Baines aliisawazishia Everton na kufanya hadi mwisho wa mchezo Man U 1, Evarton 1. Tukigeukia Hispania, Barcelona yatoka sare na Real Madrid
Nahodha wa Real Madrid alifunga katika dakika ya mwisho ya mechi na kuisawazishia timu yake na kuendeleza msururu wa kutofungwa msimu huu mbali na kuipokonya ushindi Barcelona katika mechi ya El Classico
Kichwa cha Luiz Suarez kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Neymar kiliiweka Barcelana kifua mbele katika uwanja wa nyumbani wa Nou Camp kabla ya Ramos wa Real Madrid kuzima tambo za Barcelona kwa kusawazisha kwa kichwa baada ya Luka Modric kupiga mkwaju wa adhabu na kuipatia alama moja timu hiyo inayoongoza jedwali la ligi ya Laliga.
Moja kwa moja Thom Wanjala anazungumza na Abdul Razack ambaye ni mchezaji na mchambuzi wa soka
0 maoni:
Post a Comment