Donald Trump aomba Marekani kutumia kura yake ya turufu kwenye rasimu ya UN


mediaAskari wa Israel wakimkagua Mpalestina katika mji wa al-Fawar, Ukingo wa Magharibi Agosti 16, 2016.AFP
Rais Mteule wa Marekani ameomba nchi yake kutumia kura yake ya turufu kwenye rasimu ya azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya coloni za Israel. Azimio hilo litaagiza kwamba shughuli zote za makazi hayo katika eneo hilo la Palestina, ikiwemo Jerusalem mashariki lazima zisitishwe.
Marekani imekuwa ikiunga mkono Israel katika Umoja wa Mataifa, lakini wanaounga mkono azimio hilo wamekuwa wakiaminikwamba utawala wa rais Obama utasusia kura hiyo.

"Kama Marekani inavyosema kwa muda mrefu, amani kati ya Waisrael na Wapalestina inaweza kupatiakana tu kutoka mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili, na wala si kwa njia ya masharti yanayotolewa na Umoja wa Mataifa," amesema rais mteule wa Marekani. "Marekani inapaswa kutumia kura yake ya turufu kwenye azimio lililojadiliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa." Bw Trump ameomba, wakati ambapo kura ilikua inatarajiwa Alhamisi hii saa 9h alaasiri mjini New York. Rasimu ya azimio inadai kwamba Israel iache shughuli zake za ukoloni katika maeneo ya Palestina na katika Jerusalem ya Mashariki.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amelitaka azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kusitisha ujenzi wa makaazi ya Israel katika ardhi ya Palestina.
Katika taarifa iliotolewa kabla ya kura hiyo inayotarajiwa baadaye siku ya Alhamisi, Bw Trump amesema kuwa amani haitaafikiwa kupitia hatua ya Umoja wa Mataifa kuweka masharti.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment