JPM ateua mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 22 Desemba, 2016 amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa kuwa jaji mwezi Agosti mwaka 2012
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mhe. Jaji Semistocles Kaijage anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambae muda wake wa kuwa Mwenyekiti umemalizika rasmi mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.

Jaji Mstaafu Damian Lubuva
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kipindi kingine cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.

Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid alikuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC na amemaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka 5 mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli pia amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Harold Reginald Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016. 

Jaji Harold Reginald Nsekela
Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Mstaafu Salome S. Kaganda ambae amestaafu mnamo tarehe 10 Desemba, 2016.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amewateua Majaji 4 wa Mahakama Kuu kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia leo tarehe 22 Desemba, 2016 kama ifuatavyo:-
  1. Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika
  2. Mhe. Jaji Jackobs Mwambegele
  3. Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye
  4. Mhe. Jaji Sivangilwe Sikalalilwa Mwangesi

Wateule wote waliotajwa katika taarifa hii wataapishwa kesho Ijumaa, tarehe 23 Desemba, 2016 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment