Tanzania imepanda kwa nafasi nne katika viwango vya soka duniani vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA kwa mwezi Desemba, kutoka nafasi ya 160 hadi nafasi ya 156.
Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa
Katika orodha iliyotolewa leo, Tanzania imejikusayia point 153.61 kwa mwezi Desemba ikilinganishwa na point 149 mwezi Novemba.

Katika orodha hiyo Uganda imeendelea kuwa kinara kwa Afrika Mashariki kwa kupanda nafasi moja kutoka 73 hadi 72 huku Kenya ikibaki pale pale nafasi ya 89.
Rwanda inakamata nafasi ya 92 ikiwa imepanda kwa nafasi 9 huku Burundi ikiwa nafasi ya 138 ikiwa imeporomoka kwa nafasi tano.

Kwa Bara la Afrika Senegal imeendelea kuwa kinara kwa kushika nafasi ya 33, ikifuatiwa na Ivory Coast nafasi ya 34, Tunisia nafasi ya 35 na Misri inakamata nafasi ya 36 huku Algeria ikiwa namba 5 Afrika katika nafasi ya 38.

Katika orodha hiyo, nafasi 28 dza juu duniani hazijabadilia ambapo kinara wa Soka duniani ameendelea kuwa Argentina akifuatiwa na Brazil, Ujerumani, Chile, Ubelgiji, Colombia, Ufaransa, Ureno, Uruguay na Hispania inayokamata nafasi ya 10.