KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, imemfuta kazi kocha wake


Timu ya KRC Genk ya Ubelgiji leo kupitia tovuti rasmi ya timu hiyo imetangaza kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wake mkuu Peter Maes kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo kwa mechi za hivi karibuni. 

Peter Maes anafutwa kazi ikiwa imebakia siku moja kabla ya KRC Genk kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya KAA Gent utakaochezwa kesho December 27 katika uwanja wa nyumbani wa Genk Luminus Arena.
peter-maes
Peter Maes
Uongozi wa KRC Genk umefikia maamuzi hayo ikiwa Peter Maes amedumu katika timu hiyo toka mwaka 2015, Maes mwenye umri wa miaka 52 alijiunga na KRC Genk mwaka 2015 akitokea timu ya Lokeren inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji pia.

 Genk inayochezewa na hadi inamfuta kazi kocha wake Peter Maes ipo nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji wenye timu 16.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment