Mabadiliko yaleta faraja bandari ya Dar
Mabadiliko yaliyofanywa katika bandari ya Dar es salaam yamewezesha mzigo kuongezeka katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.
Hayo yamesemwa na Meneja Mahusiano na ushirikiano wa TPA,Janeth Runzangi alipokuwa akiongea na wanahabari kutoka nchi tano zinazotumia bandari ya Dar es salaam na kusafirisha mizigo yao kupitia njia ya ukanda wa kati.
“Mzigo wa Tanzania umepanda, mzigo wa Rwanda umepanda, Mzigo wa Burundi umepanda, Malawi umepanda kwahiyo wateja wapo na bado wataendelea kutumia bandari yetu kwasababu hatujakaa tunawafuata ,” alisema Runzangi.
Nchi zinazotumia zaidi bandari hiyo n Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC),Rwanda, Burundi, Uganda ,Tanzania.
0 maoni:
Post a Comment