Mourinho ajitetea kwa kumchezesha Fellaini

jose mourinho & marouane fellaini


Jose Mourinho ametetea uamuzi wake wa kumuingiza uwanjani kiungo wa kati Marouane Fellaini kama nguvu mpya wakati wa mechi ambayo Manchester United walitoka sare na Everton Jumapili.
Fellaini alisababisha penalti muda mfupi baada yake kuingia dakika ya 85, na kuwawezesha Everton kusawazisha na mambo yakawa 1-1.
Alipoulizwa kuhusu uamuzi wake, Mourinho alisema alimwingiza kwa sababu ya kimo chake na uchezaji wa Everton.
"Nilifikiri kwamba mnafaa kuwa mnajua mengi zaidi kuhusu soka kuliko mlivyo," Mourinho alsiema akiongea na wanahabari.
"Everton si timu ya kutoa pasi kama walivyokuwa zamani. Everton ya sasa ni klabu inayocheza moja kwa moja: kipa moja kwa moja, Ashley Williams moja kwa moja, Ramiro Funes Mori moja kwa moja. Kila kitu moja kwa moja.
"Unapokuwa na mchezaji wa kimo cha mita mbili kwenye benchi unamchezesha kwenye safu ya ulinzi kuisaidia timu kushinda mipira."
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment