Kampuni ya Apple
imetangaza mipango yake ya kuunda magari yanayojiendesha. Kampuni hiyo
imekiri hayo kwa mara ya kwanza kwenye barua kwa wasimamizi wa uchukuzi
Marekani.
Apple imesema inafurahishwa sana na uwezo wa mifumo ya kutumia kompyuta kwenye maeneo mengi, "ikiwemo uchukuzi".Kampuni hiyo imesema kuna manufaa mengi ambayo yatapatikana kijamii kutoka kwa magari yanayojiendesha.
Kumekuwa na uvumi kwa muda kuhusu mipango ya kampuni hiyo, inayofahamika sana kwa kuunda simu za iPhone na kompyuta, kuunda magari yanayojiendesha.
Hata hivyo, kampuni hiyo ilikuwa haijakiri hadharani mipango hiyo.
- 'Ukinunua iPhone 7 umejifuta kazi!'
- Apple kuvutiwa na teknolojia ya magari
- Apple yaongeza bei ya laptopu na kompyuta zake
Tayari Apple imesajili anwani za tovuti mtandaoni ambazo zinahusiana na magari, zikiwemo apple.car na apple.auto.
Google tayari inafanyia majaribio magari yanayojiendesha.
Oktoba, kampuni inayounda magari yanayotumia umeme, Tesla, ilitangaza kwamba magari yake yote sasa yataundwa yakiwa na programu ya kuyawezesha kujiendesha bila kuwa na dereva.
Nchini Uingereza, gari la kujiendesha lilifanyiwa majaribio Milton Keynes majira ya joto, na majaribio zaidi yamepangiwa kufanyika London karibuni.
0 maoni:
Post a Comment