Hatimaye mgogoro uliosababisha kusimamishwa kwa uzalishaji katika
kiwanda cha saruji cha Dangote, kusini mwa Tanzania, inaelekea umekwisha
baada ya bilionea Mnigeria Aliko Dangote na Rais wa Tanzania John Pombe
Magufuli kukutana Dar es Salaam Jumamosi.
Baada ya mkutano wao Rais Magufuli na mwekezaji huyo walitokeza mbele ya waandishi wa habari katika viwanja vya Ikulu mjini Dar es salaam na wote kuhakikisha kuwa matatizo yote yaliyosababisha kusimama kwa uzalishaji yameshughulikiwa.
Baada ya mkutano wao Rais Magufuli na mwekezaji huyo walitokeza mbele ya waandishi wa habari katika viwanja vya Ikulu mjini Dar es salaam na wote kuhakikisha kuwa matatizo yote yaliyosababisha kusimama kwa uzalishaji yameshughulikiwa.
Mivutano kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Dangote ilijitokeza mwanzoni mwa Disemba baada ya kampuni hiyo kutangaza inasimamisha kwa muda uzalishaji wa saruji katika kiwanda hicho kilichopo Mtwara, kusini mwa nchi hiyo.
Baada ya uamuzi huo taarifa zilizopingana zilizuka kutoka pande mbali mbali huku ikielekea kuwa serikali inalaumiwa kwa kutoipatia kampuni hiyo ushirikiano iliyoahidi tangu awali.
Kampuni ya Dangote ambayo ni mwekezaji mkubwa katika uzalishaji saruji nchini Tanzania imekuwa ikilalamika kuwa mivutano hiyo imetokana na makosa mbali mbali ambayo inadai imeletwa na watendaji wa serikali.
Mshauri wa zamani wa mawasiliano wa Dangote, Thomas Kawogo, aliyataja baadhi ya makosa hayo ni kwa serikali kushindwa kutimiza ahadi zake kwa mwekezaji huyo. Alitoa mfano kuhusu upatikanaji rahisi wa gesi kwa kampuni hiyo ambayo inategemea gesi na makaa ya mawe katika uzalishaji wa saruji.
0 maoni:
Post a Comment