Watu 3 wahukumiwa kifungo cha miaka 73 jela kwa kosa la kuua tembo

Watu watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 73 jela kila mmoja na mahakama ya wilaya ya Serengeti kwa kosa la kupatikana na hatia ya kuingia kwenye hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Serengeti na kuua tembo.
Hukumu hiyo ilitolewa Disemba 9 mwaka huu na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Ngaile baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka. Waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo jela ni pamoja na Augen Nicodem (41) mkazi wa Mkoa wa Kigoma, Mwita Marwa (27) na Amos Alexender (25) wote wakazi wa wilaya ya Serengeti.
Hata hivyo adhabu hiyo imetokana na makosa sita ambayo yalikuwa yakiwakabili ikiwemo kusafirisha silaha kinyume cha sheria, kumiliki silaha bila kibali maalum, kuingia kwenye hifadhi bila kibali maalum, kuuwa temba na mengine mawili.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment