Wabunge wa Congress
nchini Marekani, ambao wengi wanawakilisha chama cha Republican,
wamepiga kura ya kuanza kubadilisha sheria ya Bima ya afya inayofahamika
kama Obama care iliozinduliwa na rais Barrack Obama
Bunge la seneti pia limepitisha kura hiyo, ambayo inahitaji kamati za bunge kuanza kuandika upya sheria hiyo.Hata hivyo baadhi ya wabunge wameonekana kupinga kura hiyo, wakisema ni lazima kuwe na sheria mbadala, kabla ya kufuta ObamaCare.
Hata hivyo bwana Trump anayetarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wiki ijayo, amesifu wabunge hao, na akaandika kwenye Twitter, 'ObamaCare itazikwa kwenye kaburi la sahau hivi karibuni.
0 maoni:
Post a Comment