Hawa ndio Waimbaji Watano waliotamba na Wimbo wa Kesho kwa Mwaka wa 2016.


Mwaka wa 2016 ulikuwa mwaka wa baraka kwa waimbaji wa muziki wa Injili hapa Tanzania kutokana na kila mmoja kujipatia mialiko mbalimbali na matamasha ndani  na nje ya nchi pia, Lakini kuna waimbaji kwa mwaka wa 2016 walijikuta wakiimba wimbo wenye Ujumbe unaofanana uitwao KESHO YAKO, miongoni mwa waimbaji hao ni pamoja na Bahati Bukuku, Martha Mwaipaja, Moses Simkoko, Beatrice Kitauli na PamSam, Wimbo wa Kesho yako kwa mwaka 2016 umejizolea umaaarufu mwingi kutokana na kila mmoja kuimba staili yake na yenye mvuto wake tofauti na mwingine alivyoimba.
Wa kwanza kuimba wimbo wa KESHO YAKO alikuwa Muimbaji Martha Mwaipaja ambao wimbo wake aliuita NAIONA KESHO ambao ameuimba katika staili ya ZUKU na baadhi ya maneno ambayo yamo ndani ya wimbo huo ni”Naiona kesho, kesho , iliyopangwa na Mungu. oooh kesho yakooo ooh iliyopangwa na Mungu”
Muimbaji mwingine alifuatia na wimbo wa KESHO YAKO ni Moses Simkoko ambaye wimbo wake aliuita KESHO YAKO na kwenye wimbo wake huo ulikuwa na maneno yaliyojaa ubunifu mkubwa na vionjo mbalimbali na ladha ya mziki aina ya ZUKU ambao alimshirikisha  Mwimbaji mwenzake Martin Hondwa Mathias chorus ya wimbo huo inasema”Kesho ooh kesho ooh, Kesho yako inakuuja, keshoo ooh keshoo ooh yakuinuliwa kwako
Aliyefuatia tena na wimbo wa KESHO YAKO ni Bahati Bukuku ambaye naye ameimba kwa staili ZUKU slow ndani ya wimbo wake anasema KESHO NI FUMBO baadhi ya maneno yaliyopo ndani ya wimbo huo ni “kwa waambie waje leo, leo, leo,kwa waambie waje leo, leo ,leo kwakuwa hatujui yatakayo tokeeea keshooo
Bahati Bukuku
Baada ya waimbaji hao kuimba kesho yako akatokea Mwimbaji ambaye naye anafanya vizuri na wimbo wake wa KESHO YAKO Beatrice Kitauli amefanya wimbo wa kesho na Mwimbaji mkongwe na mahiri katika Muziki wa Injili Bi.Rose Muhando Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania na baadhi ya maneno ambayo yapo kwa chorus yao yansema“Ooh la la la,Ooh la,la,la,Ooh la,la,la Naingoja kesho ,Ooh la,la,la Ooh la,la,la Ooh la,la Nikainuliwe,Ooh la,la,la Ooh la,la,la,Ooh la,la,la Nikathibitishwe
Aliyefunga Mwaka wa 2016 kwa wimbo wa KESHO YAKO ni Pam Sam aliyekuja na ZUKU ambaye naye alifanya vyema katika wimbo wake na utaalamu alioutumia wa sauti chini na kupanda kitu kilicho wafanya watu waupende wimbo wake huo wa kesho yako ambao nao unafanya vyema kwenye media  mbalimbali hapa nchini na nje ya mipaka ya Tanzania Chorus inasema ‘‘kesho yakoooo anayejua yeee*3 acheni niimbe uzuri wa baba hakuna aliye mwema zaidi ya baba,baba yangu weeeh  kajawa na baraka,baba yangu weeeh amen niko hapa,”
Hao ndio waimbaji waliotamba na vibao vyao vya KESHO YAKO na kila mmoja ameonyesha utaalamu wake katika uimbaji lakini aliyepiga muziki wa kwake peke yake ni Beatrice Kitauli aliomshirikisha Rose Muhando wengine wametumia aina moja ya muziki wa Zuku. Na kumekuwepo kwa maneno kuwa wameigana lakini kila mwimbaji amesema ameimba kutokana na Mungu alivyomuonyesha kuimba ujumbe huo maana hata Wachungaji nao huwa wanafanana jumbe zao wanapokuwa wanahubiri hivyo na wao kufanana jumbe sio dhambi ila ni nyakati tu imetokea pengine Mungu anamakusudi na ujumbe huo kwa mwaka wa 2016 sasa tutazame Jumbe ya mwaka 2017 utakuwa ni Upi?
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment