Polisi ikipiga doria katika moja ya mitaa ya mjini Bujumbura,
Polisi
ya Burundi imesema kuwa imewakamata watu watatu ikiwa ni pamoja na
mwanamke mmoja ambao inawashtumu kuhusika katika mauaji ya Waziri wa
Maji na Mazingira Emmanuel Niyonkuru.
Waziri
wa Maji na Mazingira Emmanue Niyonkuru aliuawa usiku wa kuamkia
Jumapili Januari 1, 2017 alipokua akiingia kwa gari nyumbani kwake
katika kata ya Rohero katikati mwa mji wa Bujumbura, kwa mujibu wa
polisi, huku ikiongeza kuwa aliyetekeleza mauaji hayo hajulikani aliko.Manispa ya jiji la Bujumbura inabaini kwamba mauaji ya Waziri Emmanuel Niyonkuru yaliendeshwa saa saba usiku za Afrika ya Kati.
Inaarifiwa kuwa Waziri Niyonkuru aliuawa kwa bastola.
Msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa polisi inamshikilia mwanamke aliyekua akiambatana na Waziri Niyonkuru kwa ajili ya uchunguzi.
0 maoni:
Post a Comment