ALIYEPOTOSHA TAFSIRI YA MTALII ASWEKWA RUMANDE

Muongoza watalii (Tour Guide) ambaye anadaiwa kupotosha tafsiri ya matamshi ya mtalii aliyekuwa amemaliza kufanya utalii katika Bonde la Ngorongoro mkoani Arusha amekamatwa na polisi na sasa yupo rumande.
Wiki iliyopita kupitia akaunti mbalimbali nchini Tanzania, video ya muongoza watalii huyo ilisambaa na kuwashangaza watu kwa kile alichokuwa akikisema wakati anatafsiri maneno ya shukrani na sifa njema yaliyokuwa yanatolewa ma mtalii huyo.
Mtalii huyo alikuwa akielezea kwa ufupi jinsi alivyofurahi kuwa nchini Tanzania kwakuwa sehemu alizokwenda kuziona zilikuwa zinavutia sana na Watanzania wamekuwa ni wakarimu sana kwake na wamemuonesha upendo…lakini tafsiri iliyotolewa na muongozaji wake ilikuwa inapotosha kile kilichosemwa, jambo lililopelekea Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema aliagiza muongoza watalii huyo akamatwe mara moja baada ya kuiona video hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kwamba alikamatwa katika geti la Nabi katika hifandhi ya Serengeti ambapo amewekwa rumande Mugumu.

from Blogger http://ift.tt/2kPNO53
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment