BRAD PITT AMWAMBIA MKEWE KUWA HATOMPA PESA YA MATUNZO YA WATOTO WAO!

Kwa sasa Brad Pitt na Angelina Jolie inaonekana kuwa wanakubaliana kwenye jambo moja tu maishani mwao:
Wanandoa hawa wenye mgogoro wa muda mrefu walitoa taarifa kupitia wanasheria wao wiki chache zilizopita wakisema kwamba wataweka maisha ya watoto wao mbali na vyombo vya habari mpaka pale taratibu za kuachana kwao zitakapokamilika.
Angelina Jolie na Brad Pitt
Kauli hii ilionekana kama maendeleo kwenye mgogoro wao wa kimapenzi. Ilionekana kama Jolie na Pitt wamekubaliana kuachana na wanasheria wao wanaoshughulikia masuala ya kuwaachanisha.
Lakini sasa limezuka jipya:
Mwanamama Angelina Jolie sasa anadai awe anapatiwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 223 kila mwezi kutoka kwa mumewe huyo kama pesa ya kusaidia malezi ya mtoto.
Ingawa Brad Pitt ameomba ruhusa ya Mahakama waweze kuwalea kwa zamu watoto wao sita – Maddox (15), Pax (13), Zahara (12), Shiloh (10), na mapacha Knox na Vivienne (8) – na ingawa yeye amesema kuwa “hana tatizo kuhusu kuwalea watoto,” chanzo cha habari kinasema kuwa pia anaona kiwango hiki cha pesa ni kikubwa kupita kiasi.
Brad Pitt, Angelina Jolie pamoja na watoto wao
Je, Brad Pitt ana uwezo wa kulipa kiasi hiki? Ndio.
Je, watoto wake wanastahili huduma kiasi hicho? Bila shaka.
Lakini Pitt haamini kumuachia mkewe huyu kiasi kikubwa kama hicho aamue matumizi yake mwenyewe bila kuwa na msimamizi. Pitt ndiye anatakiwa atoe pesa za matunzo ya watoto kwakuwa kwa sasa yeye ndiye mwenye kipato kikubwa zaidi kuliko mkewe.
Pitt yupo tayari kukubali kutoa kiasi hicho cha shilingi milioni 223 kila mwezi ili kugharamia mahitaji ya watoto na kuanzisha mfuko kwa ajili ya maisha ya watoto hao.
Ripoti zinasema kuwa, kila mwaka, zaidi ya shilingi milioni 558 zitawekwa kwenye mfuko wa kila mtoto, ambazo zitakuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 11 za Tanzania.
Pitt ameiambia Mahakama kwamba Jolie anapenda kutumia watoto hao kama njia ya kujipatia pesa kutoka kwake muda wowote atakaoona “atanufaika nalo” akiongeza kuwa mtalaka wake huyo “anawaanika watoto wao kwenye vyombo vya habari kwa kutaja majina ya madaktari wao na wataalamu wengine wa masuala ya akili.”
Kwa upande wa pili, Jolie amedai kuwa Pitt anataka habari kuhusu maisha ya watoto wao yawe binafsi kwakuwa anaogopa jamii itajua ukweli kuhusu yeye na anaona itamharibia jina lake.
Na ukweli huu, kwa mujibu wa Jolie, ni kwamba Pitt sio baba bora kwa watoto wao, alilewa wakiwa kwenye ndege wanasafiri mwezi Septemba mwaka jana na akampiga mtoto wao wa kiume mwenye miaka 15, Maddox.

from Blogger http://ift.tt/2losneD
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment