MAHAKAMA YAMUACHIA HURU WEMA SEPETU

Miss Tanzana mwaka 2006, Wema Isack Sepetu leo ameachiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kistu Jijini Dar es Salaam kwa dhamana ya TZS milioni 5 baada ya kuwa ameshikiliwa tangu Ijumaa juma lililopita.
Wema Sepetu ambaye anatuhumiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi nyumbani kwake ameachiwa baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili na milioni 5.
Wema Sepetu alikamatwa siku ya Ijumaa juma lililopita na upekuzi ulipofanyika nyumbani kwake alikutwa na msokoto mmoja wa bangi na karatasi maalumu za kuvutia bangi (rizla).
Wema alikuwa miongoni mwa wasanii waliotakiwa kufika kituo cha polisi kwa amri ya RC Makonda baada ya kutajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya. Baadhi ya wasanii waliachiwa jana ambapo wapo waliowekwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja huku wengine wakiwekwa chini ya uangalizi kwa miaka mitatu na kutakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kila mwezi.
Wema Spetu anatarajiwa kurudi tena mahakamani hapa Februari 22 mwaka huu baada ya majibu ya mkemia mkuu kutoka.

from Blogger http://ift.tt/2k7Utpd
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment