TUNDU LISSU AGOMA KULA NA KUHOJIWA AKISHINIKIZA KUPELEKWA MAHAKAMANI AU KUACHIWA KWA DHAMANA

CHADEMA kimesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alianza mgomo wa kula na kugoma kuhojiwa na polisi kwa mara ya pili, baada ya kutoa maelezo ya awali Jumanne. Kwa mujibu wa Peter Kibatala alisema kuwa Lissu alianza mgomo wa kula jana ili kushinikizwa kufikishwa mahakamani au kuachiwa kwa dhamana.
Kibatala alisema kuwa mke wa Lissu, Alice, alimpekea chakula jana lakini Mbunge huyo alimwambia aondoke nacho.
John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje alisema jana asubuhi polisi ilitaka kumhoji Lissu lakini akakataa kutoa maelezo.
“Lissu alikamatwa kwenye lango kuu la Bunge jioni ya Jumatatu na kusafirishwa usiku kupelekwa kituo cha kati cha Kanda Maalumu ya Polisi Dar es salaam kwa mahojiano kuhusu kauli za uchochezi kuhusu tishio la njaa nchini. “Lakini jana polisi ilitaka kumhoji juu ya maneno ambayo aliyatoa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani, Zanzibar, Januari 3. Kwa sababu ana haki ya kutokusema ama kusema, Lissu aliwajulisha polisi kuwa hana cha kusema.”
“Jana walipeleka faili kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wamekuta hana kosa, wamshtaki kwa kosa gani? DPP anatakiwa kusimamia Katiba, asiwe sehemu ya kuivunja Katiba hiyo kwakuwa ameapa kuilinda na kuitetea.”
“Kwakuwa Lissu amekaa mahabusu kwa zaidi ya saa 48 bila ya kufikishwa Mahakamani, mawakili wake jana waliwasilisha maombi Mahakama Kuu wakitaka iingilie kati.
Hatua hiyo ilifikiwa jana baada ya mawakili Kibatala na John Mallya kuwasilisha maombi hayo kwamba mteja wao tangu amekamatwa, muda wa kisheria kuwa mikononi mwa polisi umepita na pia ilitakiwa awe ameshafikishwa mahakamani ama kuachiwa kwa dhamana.
HT: @ Nipashe.

from Blogger http://ift.tt/2kwbI7a
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment